19 December 2012
Halmashauri Dar zapewa maagizo ya kuwahamisha waishio bondeni
Na Heri Shaaban
HALMASHAURI tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, zimeagizwa kuwaondoa wakazi waishio mabondeni ambao wamekaidi agizo
la Serikali kuwataka waondoke katika maeneo hatarishi.
Agizo hilo limetolewa Dar es Salaam jana na Mkuu wa Mkoa huo Bw. Meck Sadick, wakati akifungua Kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa (RCC), ambapo Wilaya hizo ni Ilala, Kinondoni na Temeke.
Alizitaka halmashauri hizo zitekeleze mkakati huo kwa kuhakikisha wananchi wote waishio katika maeneo hatarishi wanahamishwa na kupelekwa katika maeneo salama.
“Nawaagiza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na wabunge,
mdhibiti uanzishwaji makazi mapya katika maeneo hatarishi, nasikitika kusema utekelezwaji wa agizo hili, hadi sasa haujafikia kiwango cha kuridhisha,” alisema Bw. Sadick.
Alisema katika Wilaya ya Kinondoni baadhi ya wananchi wameitika agizo la Serikali ambapo zaidi ya nyumba 130 zimevunjwa ambapo katika Wilaya ya Ilala, waananchi wengi wamegoma kuondoka bondeni na kuimarisha nyumba zao.
Aliongeza kuwa, kitendo cha wakazi wa Jangwani na Bonde la Msimbazi kukaidi agizo la Serikali na kugoma kuondoka katika maeneo hatarishi kinaifanya Serikali ishindwe kufikia malengo yake.
Akizungumzia changamoto zilizopo mkoani kwake, Bw. Sadick alisema, ofisi zilizopo hazitoshelezi mahitaji ya watumishi wote wa Mkoa huo, yeye mwenyewe kukosa ofisi rasmi na uchache wa nyumba za watumishi katika mamlaka zote za Mkoa.
Changamoto nyingine Serikali kukwamisha ujenzi wa Barabara
ya Ubungo Maziwa kutokana na eneo la Jangwani kutokana na Waislamu kukataa kuhamisha Msikiti wao mbali ya kulipwa sh. milioni 75 ambazo zimewekwa katika akaunti ya Msikiti.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment