28 December 2012

Gesi ya Mtwara yaleta 'kizaazaa' *Wananchi waandamana kutaka miundombonu *Wadai kuchoshwa na ahadi zisizotekelezeka


Goodluck Hongo Dar na Cornel Antony, Mtwara

MAMIA ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara, jana walifanya maandamano ya amani kuishinikiza Serikali ijenge miundombinu
ya gesi ili iweze kuwanufaisha wananchi mkoani humo kabla ya kusafirishwa katika mikoa mingine nchini.


Maandamano hayo ya kihistorria yalianza saa tatu asubuhi katika Mtaa wa Mtawanya kupitia Barabara ya Magomeni, Soku Kuu, Bima na kuishia katika Viwanja vya Mashujaa.

Katibu wa Umoja wa Vyama vya Siasa mkoani humo, Bw. Seleman Litope, ndiye aliyeyapokea katika uwanja huo na yalipata baraka za Jeshi la Polisi ambao walikuwa wakilinda usalama.

Akihutubia waandamanaji, Bw. Litope alisema lazima wakazi wa Mtwara wajue haki zao kuhusu nishati hiyo na jinsi wanavyoweza kufainika nayo kwani gesi hiyo inachimbwa mkoani humo lakini miundombinu yake inajengwa sehemu nyingine.

Mmoja kati ya waandamanaji hao, Bw. Joseph Siraji, alisema wakazi wa Mkoa huo wamekosa maendeleo kwa muda mrefu
na wamekuwa wakifanywa watoto licha ya kuchimbwa gesi
hiyo mkoani humo lakini dalili zinaonesha watakaonufaika
si wananchi wazawa bali kutoka mikoa mingine nchini.

“Serikali imekuwa ikitufanya watoto wadogo sisi wakazi wa Mkoa huu kwa kutuambia gesi hii itawanufaisha wazawa lakini matokeo yake ni tofauti na ilivyo sasa,” alisema Bw. Siraji.

Katika maandamano hayo, wananchi walisema wao hawapingi kusafirishwa kwa gesi hiyo bali wanachotaka ni kujengewa miundombinu ambayo itawawezesha kufaidika nayo.

Walidai awali Serikali iliwaahidi kupata umeme kwa bei rahisi
badala yake, waliojenga mita 30 kutoka barabarani ndio wananufaika na punguzo hilo hivyo wao wanaamini Serikali iliwadanganya kuwa itashusha gharama za umeme.

Maandamano hayo yaliwajumuisha wafuasi wa vyama vya siasa kutoka CUF, TLP, CHADEMA na SAU iaispokuwa wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), ambao hawakushiriki.

Awali maandamano hayo yalitakiwa kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia lakini aliyakataa kwa madai yamefanyika siku ya kazi.

18 comments:

  1. Chadema imemwaga sumu tena! Gesi si suala la Tanzania ila la Mtwara! Ni kweli hali yao ya maisha yapaswa kuimarishwa na kuboreshwa. Lakini Tanzania bado haijawa na mfumo wa majimbo. Ndizi, mihogo, viazi, dagaa, samaki nk. vyote huenda Dar. Dar ni mkusanyiko wa watanzania wote na ndicho kitovu cha uchumi na biashara.Suala ni kwamba Mtwara itafaidikaje na pia sehemu nyingine za nchi zinazochangia uchumi kwa shughuli nyingine zitafaidigaje. La sivyo nchi itagwanyika vipandevipande.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtazamo wako kuwa CHADEMA kuwa wamemwaga sumu hauna mashiko kabisa.UKWELI hebu ona Gesi ya Songosongo haijawanufaisha watu wa huko,ona uchumi wa watu wanaoishi kuzunguka migodi walivyo masikini Au labda nimuulize mbona viwanda vya kuchakata Sangara havijajengwa Dar?.Naona wewe hujuwi kitu ila unalishwa kitu cha kuongea.

      Delete
  2. NI VIZURI WATANZANIA TUACHE KULISHWA CHUKI NA UHOCHEZI ILI AMANI YA NCHI IVURUGIKE WAKATI TUKIPATA UHURU MAUZO YA NJE YALITEGEMEA ZAIDI ZAO LA MKONGE,PAMBA, KAHAWA NA MADINI YA ALMAS TOKA MWADUI NA DHAHABU TOKA GEITA MAPATO YALIYOPATIKANA YALITUMIKA KUFUTA UJINGA,KUPAMBANA NA MARADHI NA KUONDOA UMASKINI SIO MAENEO RASILIMALI HIZO ZILIKUWA ZINAPATIKANA TU BALI NI TANZANIA YOTE BILA HIVYO MAENEO HAYO YANGEKUWA YAMEKUWA KIELIMU NA VYUO VIKUU VINGI,HOSPITALI ZA RUFAA NYINGI,VIWANDA VIKUBWA VYA KUZALISHA MITAMBO HAIKUWA HIVYO KWANI MAPATO YALIELEKEZWA TANZANIA NZIMA UNAPOKUTANA NA MAZUZU WALIOFILISIKA KIMAWAZO WAKAPANDA MBEGU ZA KUSAMBARATISHA NCHI IKIZINGATIWA LEO HAKUNA MWENYE BUSARA NA HEKIMA WA KUGUNDUA KUWA WAKO MABEBERU NA WAKOLONI NI WEUSI NGOZI ILA NI MABEBERU NA WAKOLONI WANAFADHILIWA NA MABEBERU NA WAKOLONI INAPOFIKIA WAKOLONI NA MABEBERU WANAOFADHILIWA KUTOKA NJE TUNASHINDWA KUWAONA NCHI HII ITASAMBARATIKA

    ReplyDelete
  3. MHESHIMIWA ALIYECHANGIA KABLE YANGU NAONA ANAENDEKEZA SIASA ZAIDI KULIKO UKWELI NA HOJA ILIYOPO MEZANI.HAPA WANANCHI WA MTWARA JAMANI WANACHODAI NI KWANZA WAO WENYE KUWA NA RASIMALI HII MKOANI KWAO WAWEKEWE MIUNDOMBINU YA KUPATA KWANZA HUDUMA HII NDIPO ITOKE NJE HILI HALIPINGINGI NA NDIO UKWELI ULIVYO.

    KUMALIZA HII EBU SERIKALI YETU SIKIVU MALIZA TATIZO LAO ELEKEZA WAKANDARASI WAJENGE MIUNDOMBINU MTWARA AU KAMA IMO KATIKA MKATABA BASI WANANCHI WAELIMISHWE UJENZI HUO UTAFANYIKA KULIKO WAZIRI KUKIMBILIA MASUALA YA AMANI NA UTULIVU HII HAINA SENSE JIBU HOJA YA WANANCHI MH WAZIRI IKIAMBATANA NA UTEKELEZAJI WA UJENZI NA MATAKWA YA WANANCHI HAO.HAYA MAMBO YAMEANZA SIKU NYINGI MFANO DHAHABU YA GEITA/KAHAMA IMENUFAISHA VIPI MIKOA/WILAYA HUSIKA.MWADUI KUNA ALMASI IMENUFAISHA VIPI SHINYANGA NA KITONGOJI CHA MAGANZO BADO WANANCHI NI DUNI NA HUDUMA ZA JAMII NI MBOVU KUFA MTU.
    TUJENGE UTAMADUNI WA KUWA WAKWELI NA SIO SIASA KILA JAMBO.

    ReplyDelete
    Replies
    1. HUJAJIBU HOJA HATA WANGEPEWA UMEME WA BURE AU HATA GESI YA BURE ITATUMIKA KWENYE NYUMBA ZA MAJANI SHIDA MIKOA HIYO WAKATI MIKOA YA KASKAZINI IKIWEKEZA KWENYE ELIMU WALIKUWA WAKIWEKEZA KATIKA NGOMA HATA LEO TUU UTAFITI MDOGO TU MIKOA YENYE SHULE ZA SEKONDARI ZA KATA NI IPI ???? JE WATAKAOKWENDA HIGH SCHOOL WENGI NI WA MIKOA IPI?? JE WATAKAOJAZA NAFASI ZA CHUO KIKUU NI WA MIKOA IPI??? JE RASILIMALIWATU ITAKAYOAJIRIKA NI IPI???? SIDHANI MIKOA ILIYOPIGA HATUA KATIKA ELIMU NA MAENDELEO\[WALIWEKEZA] NI RAHISI KUHAMASIKA KUFANYA MAANDAMANO YA KIPUUZI ;NAWASHANGAA WANAOHAMASISHA MAANDAMANO HAYA WANAUTAKA URAIS TULOGWE TUWAPE HATA IKULU ITAHAMISHIWA NYUMBANI KWAO UPEO MFUPI WA KUONA MBALI MBONA OBAMA HAJAJENGA MABARABARA YA KENYA TUACHE UPUUZI

      Delete
    2. pumbaaaaaaaaaaaaaaa

      Delete
  4. WANAINCHI WA MTWARA NA VIUNGA VYAKE WANA HOJA YA "MSINGI"KABISA.KIKUBWA SELIKALI IACHE KUTOA AHADI AMBAZO HAZITEKELEZEKI.PIA HAILETI MANTIKI KINU CHA KUFUA UMEME KUJENGWA NJE YA MKOA HUO NA KUFANYA HIVYO NI KUWANYIMA FURSA ZA KIUWEKEZAJI NA MAENDELEO KWA UJUMLA WAKE WAKAZI WA MIKOA YA KUSINI.MTWARA KWANZA NA TAIFA BADAE KAMA ILIVYOFANYIKA KWA MIRADI MINGINE KTK MIKOA MBALIMBALI.HUSHINDWA KUFANYA HAYO NI KULIGAWA TAIFA NA GHARAMA ZAKE NZITO KWA TAIFA.SERIKALI ILITAMBUE HILO KAMA VIONGOZI NA WADAU MBALIMBALI WANAVYOCHANGIA HOJA HIHO YA MSINGI KWA WALALAMIKAJI.wachangiaji achane ushabiki na kubeza kwa lugha mbaya.TUSOME ALAMA ZA NYAKATI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ukikosa uelewa unakua mtu wa matata siku zote. Huelewi mabo ndio sababu unasema Mtwara kwanza utaifa baadaye. Unataka watu wa mtwara waende mikoa mingine kwa paspoti vile mtwara kwanza? Mambo ya msingi yapo yakujadiliwa.
      hakuna anayeyazuia. Kuna fidia, kuna tasmini za uharibifu wa mazingira, kuna huduma za jamii. Yote hayo yanajadilika usifikiri wengine hawana uelewa. Lakini wewe unachochea fujo tu. Gesi yenyewe hata haijauzwa!

      Delete
    2. WEWE NI MWELEWA NA SI HAWA WENGINE WANAJALI SIASA ZAIDI KULIKO UKWELI ULIOPO ETI WANATAJA UKASKAZINI HAPA SUALA SIO UKASKAZINI WANANCHI WA MTWARA WAMEANZA MIKOA MINGINE PIA WATAZINDUKA AMBAKO PIA KUNA RASILIMALI AMBAZO HAZIWANUFAISHI WANANCHI WA ENEO HUSIKA. JAMANI MSI COMMENT ILI MRADI UONEKANE UMECOMMENT

      Delete
  5. Acheni ujinga bali jadilini hoja zenye mashiko. Hivi serikali itapata hasara gani kama watajenga mitambo ya kufua umeme Mtwara mahali ambapo malighafi hiyo inapatikana? Tunachotaka watu wa Mtwara ni kujengwa kwa kiwanda hicho huku kwetu kisha hiyo gesi isafirishwe hadi Dar es salaam na maeneo mengine ya nchi kwa ajili ya matumizi. Nyie mazezeta mnaodai kuwa kuwa rasilimali za nchi zinanufaisha wananchi wote ni kweli? Kama ni kweli mbona haipo hivyo? Kwa mfano umeme wa Mtera unawanufaishaje wananchi wa Songea ambao muda wote wapo gizani kutokana na tatizo la umeme? Je,siku Jumuiya ya Afrika Mashariki ikianza na nchi kama Kenya/Uganda wakija kuhamisha raslimali zetu eg.gesi tusije kuhoji kwasababu zitakuwa zinztumika ndni ya Jumuiya?

    ReplyDelete
  6. Yote juu ya hayo yote bado serikali inabidi ikubali kwamba haki za wana kusini haijaliwi mfano ni daraja la Nangoo Masasi lilikatika miaka ya tisini hadi hivi karibuni ndo limeanza kujengwa .kupitia mfano huo daraja lingekuwa la mto Wami hali ingekuwa kama hii.Oneni aibu na soni machoni toeni elimu na hatimae mtaona matunda yake.

    ReplyDelete
  7. NI KWELI KILA MTU ANA UHURU WA KUTOA MAWAZO YAKE ILIMRADI ANAYAONA YANAFAA WAACHENI WATOE MAWAZO YAO.lEO MTWARA GESI IBAKI KWAO, KESHO RUKWA,MBEYA,RUVUMA NA IRINGA WATADAI VYAKULA WANAVYOZALISHA WAUZE ZAMBIA MALAWI NA KONGO VISIPELEKWE DAR.SIKU NYINGINE NAPO GEITA, MERERANI,MWADUI NA MCHUCHUMA NAO WATASEMA FEDHA ZA MADINI ZOTE ZIBAKI KWAO .JAMANI TUNAELEKEA WAPI TUSITAFUTE HALI TUSIYOWEZA KUIHIMILI.MAANA YAKIANZA TU SIE TULIOANDAMANA NDIO TUTAKAOATHIRIKA NADHANI SASA SIASA BASI NI VITENDO TU

    ReplyDelete
  8. Tanzania ni ya watanzania na kila sehemu ni mahali pazuri pa kuwekeza nradi kuwepo na Umeme na barabara

    Nilipopangiwa kufanya kazi Mtwara miaka ya themanini kwanza kabisa nilikata tamaa kwani hata barabara ya kufika huko ilikuwa haiaminiki

    Ilinilazimu kutumia takribani wiki hadi kufika Mnazi mmoja Lindi ambako kilikuwa ndio kituo changu cha kazi.Baada ya hapo usafiri wa kwenda na kurudi nililazimika kutumia ndege

    Nilitamani sana kuwa na makazi ya kudumu huko lakini tatizo kubwa lilikuwa ni usafiri na umeme na kitoweyo hasa nyama ya ngombe.

    Lakini kwa watu walikuwa na subira wanafaidi matunda ya sra za chama na serikali kwani sasa barabara ya lami imejengwa, umeme unapatikana na kubwa zaidi hata viwanda vinaanzwa kujengwa kama kiwanda cha saruji

    Kupatikana kwa gesi katika mkoa wa Mtwara kungeifanya Mtwara iwe makao makuu ya mikoa ya kusini kwa kuleta maendeleo kwani ina ardhi nzuri yenye rutuba, ina bandari ni swala la kuwapa mikopo wananchi na kujenga nyumba zilizo bora na wawekezaji wengi kuwekeza huko badala ya kuanza kufikiria kuhamamisha Gesi hiyo na kuipeleka Dar kwanza na kuwaacha wananchi wa maeneo hayo na umaskini wao

    Kweli tunaihitaji gesi Dar lakini ipo gesi nyingi ya Songosongo bado haijaanza kutumika vizuri aidha eneo la Temeke kuna tetesi za kuwepo na gesi nyingi sana

    Mimi kwa maoni yangu ningeona ni bora kuujenga mji wa Mtwara na kuweka miundo mbinu yote ili watu wawekeze na baadaye kuipeleka gesi sehemu nyingine kama kujenga Gridi nyingine ya Taifa kuanzia Mtwara na kuelekea mikoa ya Songea Mbeya, Rukwa na hadi Tabora kwa maendeleo ya sehemu hizo pia

    Na gesi ya Songosongo itumike kwenye mikoa ya Dar pamoja na itakayo vumbuliwa Temeke wajenge tena Gridi nyingine kuelekea Dodoma Singida Shinyanga na Mwanza

    Kwa maana nyingine kuwepo na mipango thabiti ya kutumia vizuri raslimali hizi za Taifa kwa manufaa ya watanzania wote na siyo kwa wachache Najua kuwa yapo maeneo kama Ludewa nayo yanaweza kujenga Gridi nyingine kwa uzalishaji wa makaa ya mawe, na Songea na Singida wanaweza kutumia Urani kuzalisha umeme pia na kuungiza kwenye Gridi ya taifa

    Nampongeza Raisi Kikwete kwa kukubali kusikiliza kilo cha wana Mtwara katika salamu za MWAKA MPYA

    Mungu ibariki Tanzania na watu wake

    ReplyDelete
  9. WEWE ANZISHA TU SERA ZA MGAWANYIKO, UKIFANIKIWA HILI, SISI WATU WA MKOA WANGU TUTATAKA TUTAWALIWE KWANZA NA WA MKOA WETU KWANZA WA MIKOA MINGINE BADAYE

    ReplyDelete
  10. haya ndio maendeleo na nchi zote zenye ugomvi na mapigano tatizo kubwa ni rasilimali kama hizo tuombe mungu aiepushae tanzania tusiingie kwenye migogoro atupe fikra sahihi za kutatua na kujua nini kiwe cha kwanza scale of preference ili kuhakikisha kila kitu kinalea tanzania

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sijui ni rais yupi wa kulaumiwa kwa kuwaonea wananchi wa Mtwara. Nyrere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete? Ama mbaya ni aliyeanzisha tafiti za mafuta na gesi? Wote wanasema Mtwara lazima iangaliwe ndani ya maslahi ya taifa. Hiyo ndio kauli sahihi. Nchi zote zenye kazalisha mafuta huyasafirisha kwa mabomba kufikia masoko ya ndani na nje. Kama huamini soma tu jiografia ya nchi zenye kuzalisha bidhaa hizo. Ushaelezwa gesi ni nyingi sana kiasi cha kwamba Mtwanza itatumia kiasi kidogo tu. Sasa mitungi ya gesi ijazwe Mtwara ipelekwe dar badala ya kutumia bomba? Grid ya umeme ianzishwe Mtwara ni sahihi sana. Gesi ya ya ziada ipelekwe kwa bomba kwenya soko kuu. Hili ni sawa pia. Wananchi wa Mtwara wako sahihi. Tusiwachanganye kisiasa.

      Delete
    2. DAR INACHANGIA ASILIMIA KUBWA KWA TAIFA, HIVYO MAMBO KAMA YA ELIMU NA ULINZI PIA WAPATIWE KWANZA WAO. MIKOA INAYOTOA WANASIASA WENGI PIA WATAWALE KWANZA KWAO

      Delete
  11. Gesi Ikienda Dar kuna tatizo gani?-
    Gesi ikienda Dar kuna faida gani?-faida ya kubakiza gesi Mtwara ni ipi kesho na kesho kutwa Kigoma itataka kitu fulani...Zanzibar wata sema yao...Kilimanjaro watataka kilimanjaro...Tamaaa..

    ReplyDelete