04 December 2012

DC: Viongozi wa dini msibeze maendeleo


Na Faida Muyomba, Geita

MKUU wa Wilaya Geita, Bw. Manzie Mangochie, amewaonya viongozi wa dini wanaodharau shughuli za miradi ya maendeleo kuacha mara moja kwani hawatendi haki kwa waumini wao.

Bw. Mangochie aliyasema hayo juzi katika uzinduzi wa
albamu ya kwaya ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu.

“Wapo baadhi ya viongozi wa dini nchini ambao wamekuwa mstari wa mbele kubeza shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na Serikali kutokana na matakwa yao binafsi, upotoshaji wa namna hii haukubaliki,” alisema Bw. Mangochie.

Aliongeza kuwa, viongozi hao wanapaswa kuangalia shughuli ngapi za maendeleo zimefanywa na Serikali badala ya kubeza kila jambo kwani kufanya hivyo ni kuwakatisha tamaa wananchi.

Aliahidi kuwa bega kwa bega na viongozi wa kwaya hiyo ili kuhakikisha inasonga mbele katika safari zake za kueneza neno
la Mungu kutokana na mchango wao mkubwa wenye lengo la kudumisha amani nchini.

Awali mlezi wa kwaya hiyo, Ladislaus Mwesa, katika risala yake kwa Bw. Mangochie, alisema yapo mambo mengi ambayo yanawakabili hususan kipato duni.

“Kwaya yetu ina kabiliwa na matatizo mengi, tumekuwa imekuwa ikitegemea msaada kutoka kwa walezi, wafadhili na watu wachache wenye mapenzi mema, hatuna miradi inayoweza kutuongezea kipato,” alisema.

Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo, wameazimia kutumia njia
ya uimbaji kufikisha ujumbe wa Mungu kwa wananchi na wanatarajia kununua vifaa vya usafiri kama vile gari ili
waweze kurahisisha kazi zao.

Katika uzinduzi huo, kwaya hiyo ilifanikiwa kukusanya fedha taslimu sh. milioni 2.5 na ahadi sh. milioni 1.7 ambapo Bw.
Mangochie alichangia sh. 560,000.

1 comment:

  1. VIONGOZI WENGI WANA HASIRA NA SERIKALI KWANI AWALI MISAADA MINGI YA WAFADILI ILIINGIA NCHINI ILI IPELEKWE KWENNYE MASHULE,HOSPITALI,NA HUDUMA NYINGINEZO ZA JAMII ILIKUWA HAILIPIWI KODI IKITEGEMEWA ITAWAFIKIA WALENGWA BADALA YAKE UFISADI WA KUTISHA ULIKUKWA UKIFANYIKA WAKIDANGANGANYA WAUMINI WAFUMBE MACHO WASALI KUMBE WANAIBIWA SERIKALI ILIPOGUNDUA NA KUTOZA MISAADA HIYO KODI NDIKO UGOMVI ULIKOANZIA SASA HIVI KUNAMICHANGO KWENYE TAASISI ZA DINI YA KIFISAFISADI MADHALI HAIKAGULIWI HAIHOJIWI INAISHIA MATUMBONI MWAA VIONGOZI WA DINI BADALA YA KUWAHUDUMIA WAUMINI MFANO HAKUNA NAFUU KWENYE HUDUMA ZA ELIMU, AFYA N.K

    ReplyDelete