03 December 2012

C: Ngono katika kambi za uvuvi marufuku


Na Jovither Kaijage, Ukerewe

MKUU wa Wilaya ya Ukerewe, mkoani Mwanza Bi. Mery Tesha, apiga marufuku biashara ya ngono wilayani humo hasa katika kambi za uvuvi ili kuzuia maambukizo mapya ya ugonjwa wa UKIMWI.


Bi. Tesha aliyasema hayo juzi mjini Nansio, katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyiika katika Uwanja wa Mongera na kuzizitiza kuwa, vitendo hivyo vimekuwa chanzo kikubwa cha mahambukizo mapya.

Alisema jamii kubwa haifurahishwi na biashara hiyo na kuonya yeyote ambaye atakwenda katika kambi za uvuvi bila shughuri maalumu atakamatwa kwa kosa la uzululaji na kushtakiwa.

Aliongeza kuwa, uchunguzi aliofanya muda mrefu amebaini wapo baadhi ya wanawake wanaokwenda katika kambi za hizo ili kufanya biashara haramu ya ngono ambapo mbali ya kukiuka mahadili ya Mtanzania ndio chanzo kikuu cha mahambukizo ya ugonjwa huo.

Bi. Tesha alilazimika kutoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa ya hali ya mahambukizo ya UKIMWI ambayo iliandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii iliyosomwa na Bw. Novatus Gabriel.

Pamoja na mambo mengine, taarifa hiyo ilidai kuwa kitendo cha baadhi ya wanawake mjini humo kufanya biashara ya ngono katika kambi za uvuvi kinachangia maambukizo mapya wilayani humo.


“Hadi kufikia Novemba mwaaka huu, watu 17,227 wamepima
afya zao wilayani hapa na kati yao, 507 wameathilika wakiwemo wanawake 316.

“Wagonjwa walioathirika hadi Novemba mwaka huu wameongezeka na kufikia 410, waanaopewa dawa za
ARVs kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI hadi
sasa ni 2,209,” alisema Bw. Gabriel.

Alisema vifo vilivyotokana na ugonjwa huo vimeongezeka ambapo mwaka 2011, walikuwa 30 na mwaka huu watu 65 wamepoteza maisha wengi wao wakiwa wanawake.

Hata hivyo, Bw. Gabriel alisema juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo zinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa
wataalam, bajeti finyu isiyofika kwa wakati na matumizi mabaya
ya teknojia ya mawasilino kama simu na intaneti hasa kwa vijana.

No comments:

Post a Comment