28 December 2012
Bodi NBC yaridhia kujiuzulu Marufu
Na Mwandishi Wetu
BODI ya Benki ya NBC Tanzania, imethibitisha na kuridhia kujiuzulu kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw.
Lawrence Mafuru, kuanzia Desemba 31 mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, imesema Bw. Mafuru alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki
hiyo tangu Juni mosi 2010.
Bodi hiyo iliahidi kumtangaza mtu ambaye atachukua nafasi ya Bw. Marufu baada ya kupokea idhini ya udhibiti na kumpa shukrani nyingi kwa mchango alioutoa katika benki hiyo yenye uzoefu
wa miaka 45 katika kutoa huduma za kifedha nchini.
Ilimtakia Bw. Mafuru mafanikio mema baada ya kujiunga na
benki hiyo Agosti 2007 kama Mkuu wa Hazina na baadae
kuwa Mkurugenzi Mtendaji.
NBC ni moja ya benki inayotoa huduma za rejareja za kibenki
kwa wateja wengi nchini ikiwa na matawi 52 nchi nzima
na wafanyakazi 1,200.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment