03 December 2012

ATIME yashiriki maonyesho ya Jua Kali Burundi


Na Heri Shaaban

CHAMA Chama Tiba Asili na Tiba Mbadala Tanzania (ATIME) imepeleka watoa tiba asili wanne kutoka Tanzania kushiriki katika Maonyesho ya 13 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (JUA KALI)nchini Burundi.


Maonesho hayo ya Jua Kali ambayo yalianza Desemba Mosi, mwaka huu yatafanyika kwa muda wa wiki moja katika nchi hiyo,ambapo kwa Tanzania imewakirishwa na watoa tiba asili wanne.

Akizunguza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,Mjumbe wa ATIME Taifa Othiman Elia alisema kuwa kwa Tanzania inawakilishwa na Mikoa miwili ya Dar es Salaam na Mbeya.

Madhumuni ya kushiriki katika maonesho hayo kuimarisha umoja na mshikamano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kubadilishana uzoefu wa kitabibu na dawa miongoni mwa watabibu wa kiafrika ambapo awali maonyesho hayo yalifanyika mwaka 1999 mkoani Arusha kwa kutiliana saini mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alisema kuwa tafiti zinaonyesha kuwa tiba asili inatumiwa na Watanzania asilimia 60 hadi 65 kutokana na kuwa na uwezo wa kuhimili magonjwa sugu kama kisukali na pumu.

Kwa upande wake mmoja watu waliobatika katika safari hiyo, Mkurugenzi wa Boresa Medical Trading Boniventura Mwalongo kutoka Mbeya alisema kuwa wanauzoefu wa kutibu magonjwa kwa usahii ambayo hospitali hayapati nafasi.

Naye Mwenyekiti wa ATIME Simba Simba alisema kuwa chama hicho mpaka sasa kina wanachama hai 6000 katika mikoa yote Tanzania na wanaendelea kuwapa elimu ya kutosha ili waweze kuwa mabalozi wa watabibu wengine.

No comments:

Post a Comment