19 December 2012
Abiria 39 wajeruhiwa katika ajali
Na Jesca Kileo
WATU 39 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela, alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa nne asubuhi katika barabara
ya Morogoro eneo ya Kiluvya Gogoni, wilayani Kinondoni.
Alisema gari yenye namba T 354 AJZ, aina ya Toyota Corolla, iliyokuwa ikiendeshwa na Bw. Vicent Massawe akitokea Kihaba kijijini kwenda mjini, iligongana na gari yenye namba T 607 BDB, aina ya Toyota Coastal, iliyokuwa ikiendeshwa na Tumsifu Mushi akitokea Ubungo kwenda Kibaha.
Aliongeza kuwa, gari yenye namba T 607 BDB, ilipoteza mwelekeo na kuligonga gari jingine lenye namba T 921 BNC, aina ya Toyota Coastal, iliyokuwa inaendeshwa na dereva ambaye hakufahamika akitokea Kihaba kwenda Ubungo.
“Katika ajali hii, abiria 39 walipata majeraha sehemu mbalimbali za mwili na walikimbizwa katika Hospitali ya Tumbi Kibaha na wote walitibiwa na kuruhusiwa.
Alisema gari iliyosababisha ajali hiyo ipo kwenye Kituo cha Polisi Osterbay na upelelezi unaendelea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment