27 December 2012

143 wazaliwa mkesha wa Krismasi Dar



David John na Heri Shaaban

JUMLA ya watoto 143, wamezaliwa kwenye mkesha wa Sikukuu ya Krismasi katika Hospitali za Amana, Temeke, Mwananyamala na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), zote za Dar es salaam.


Kati ya watoto hao, 53 wamezaliwa katika Hospitali ya Temeke, Mwanaynayama (25), Amana (62) na Muhimbili watatu.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Amana, Bi. Upendo Kitaponda alisema kati ya watoto 62, sita walizaliwa kwa operesheni.

“Hali za watoto na mama zao zinaendelea vizuri, kati ya watoto waliozaliwa wanaume 32, wanawake 30,” alisema Bi. Kitaponda.

Naye Ofisa Msimamizi upande wa Uuguzi katika Hospitali ya Temeke, Bi. Asha Kitumbuizi, kati ya watoto 53 waliozaliwa,
wanaume 29, wanawake 24, mzazi mmoja amejifungua mapacha.

Alitoa wito kwa wanawake kufuata maelekezo wanayopewa wanapokuwa wajawazito pamoja na kwenda kujifungua katika
hospitali ambako huduma za uzazi hutolewa bure.

Naye Muuguzi wa Hospiatali ya Mwananyamala, Anjew Magesa alisema kati ya watoto 25 waliozaliwa, waanawake 10, wanaume
15 na hakuna aliyejifungua kwa operesheni.

Katika Hospitali ya Muhimbili, kati ya watoto watatu waliozaliwa  wakiume wawili na mwanamke mmoja kwa mujibu wa Ofisa Habari wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha.

No comments:

Post a Comment