26 November 2012

Wananchi Gezaulole wadaiwa kunywa maji ya kemikali

 Na.Lilian Justice,
 Kilosa.

WANANCHI wanaoishi katika maeneo ya Gezaulole  nyumba namba 30, 38 katika mji mdogo wa Ruaha Wilayani Kilosa  mkoani Morogoro wanakabiliwa na ukosefu wa maji safi na hivyo kupelekea kunywa maji ya kemikali yatokayo kiwandani.




Hayo yalibainishwa na Mmoja wa wakazi wa eneo hilo Bw. Andrew Trygol  wakati akizungumza na gazeti hili ambapo alisema kuwa kero hiyo ya ukosefu wa maji safi ni ya muda mrefu ambapo hadi kufikia hivi sasa ni miaka mitano.



Trygol alisema kuwa  wananchi wa maeneo hayo hulazimika kunywa maji machafu  yanayotoa katika  kiwanda cha sukari cha K2 ambapo ni  Kilombero  sugar kilichopo katika mji mdogo wa Ruaha.



Aidha alisema kuwa  kutokana na wananchi kutumia maji hayo wamekuwa wakikumbwa na changamoto mbambalimbali ikiwemo kupatwa na magonjwa ya homa ya matumbo,kuhara damu na hata  wengine kupoteza maisha.



‘’Maji hayo machafu yameleta athari kubwa na hasa watumiaji kutoka Block 30-38 hivyo tunaiomba mamalaka husika au serikali kuliangalia suala hili kwa  umakini zaidi ili kulipatia ufumbuzi wa kudumua kwani tatizo hilo lilianza tangu mwaka 2000‘’alisema Bw. Trygol.



Pia alisema kuwa wananchi wanaoishi katika block 30,31 na 32 hawana uwezo mkubwa kifedha na ni maskini ambapo huwa ndio wanaolinda  kiwanda na wengine ni wasafirishaji wa miwa kutoka mashambani.



Hata hivyo alisema kuwa licha ya kuwepo kwa mto Ruaha bado mto huo maji yake sio salama kwa matumizi ya binadamu   kutokana na kuwepo kwa kemikali na maji kubadilika rangi ya manjano jambo ambalo ni hatari kwa wananchi wanaojaribu kutumia maji hayo.


No comments:

Post a Comment