29 November 2012

Vodacom yazindua duka la mauzo DarNa Darlin Said

KAMPUNI ya Vodacom imezindua duka jipya la mauzo ambalo litasaidia kupunguza msongamano wa wateja kwenye maduka mengine.

Uzinduzi huo uliofanyika Dar es Salaam jana ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rubenanga .

Rubenanga alisema kutokana na jiji hilo kukua kwa kasi mahitaji pia yameongezeka, hivyo ni wajibu wa kampuni husika kuhakikisha zinatoa huduma zitakazoendana na mahitaji ya wateja.

Mbali na hilo alisema huduma za kampuni za Vodacom ni bora na za uhakika kwani inatoa huduma bora za kifedha ya Mpesa inayowasaidia Watanzania wengi na wasio na akaunti za Kibenki.

Awali alisema Serikali inaunga mkono kampuni hiyo kwa jitihada zake za kurahisisha mawasiliano kwa Watanzania ikiwa ni moja ya lengo lake la kuwaunganisha wananchi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Rene Meza, alisema wanajivunia kufungua duka hilo kwani wametengeneza ajira mpya.

Alisema hadi kufikia sasa Vodacom imetoa ajira za moja kwa moja kwa moja kwa wafanyakazi 500 na wengine zaidi ya 3,000 wana ajira zisizo rasmi.  
Na Darlin Said

KAMPUNI ya Vodacom imezindua duka jipya la mauzo ambalo litasaidia kupunguza msongamano wa wateja kwenye maduka mengine.

Uzinduzi huo uliofanyika Dar es Salaam jana ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rubenanga .

Rubenanga alisema kutokana na jiji hilo kukua kwa kasi mahitaji pia yameongezeka, hivyo ni wajibu wa kampuni husika kuhakikisha zinatoa huduma zitakazoendana na mahitaji ya wateja.

Mbali na hilo alisema huduma za kampuni za Vodacom ni bora na za uhakika kwani inatoa huduma bora za kifedha ya Mpesa inayowasaidia Watanzania wengi na wasio na akaunti za Kibenki.

Awali alisema Serikali inaunga mkono kampuni hiyo kwa jitihada zake za kurahisisha mawasiliano kwa Watanzania ikiwa ni moja ya lengo lake la kuwaunganisha wananchi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Rene Meza, alisema wanajivunia kufungua duka hilo kwani wametengeneza ajira mpya.

Alisema hadi kufikia sasa Vodacom imetoa ajira za moja kwa moja kwa moja kwa wafanyakazi 500 na wengine zaidi ya 3,000 wana ajira zisizo rasmi.  No comments:

Post a Comment