27 November 2012

Serikali mtegoni waliofuja bil. 86/- *Mnyika aahidi 'kuwaanika' wahusika *Adai ni sehemu ya ufisadi mkubwa


Na Eckland Mwaffisi

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, Bw. John Mnyika, amesema wizi wa sh. bilioni 86, unaodaiwa kufanywa na watumishi wa Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ni sehemu ya ufisadi mkubwa katika utekelezaji wa Mpango wa Serikali wa kufua umeme wa dharura.

Bw. Mnyika aliyasema hayo katika mahojiano na gazeti hili juu ya msimamo wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ambaye katika tarifa yake kwa vyombo vya habari juzi, alisema wananchi wanapaswa kuelezwa kinaga ubaga kinachoendelea katika sekta ndogo ya umeme nchini.

Alisema anaungana na Bw. Kabwe kumtaka Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, kuueleza umma juu ya fedha ambazo Hazina imezitoa kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura kati ya Novemba 2011 hadi Oktoba mwaka 2012.

Bw. Mnyika ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, alimtaka Waziri wa Nishati, Profesa Sospeter Muhongo na taarifa
ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Seerikali (CAG), kuwekwa hadharani juu ya suala hilo.

“Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), nayo

kuhusu matumizi ya Bw. John Mnyika katika hotuba yake ya Bajeti ya Wizara hiyo mwaka 2011, naye alipendekeza ufanyike uchunguzi kuhusu kashfa hiyo lakini
juhudi zote hazikuzaa matunda.

Bw. Kabwe ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani bungeni na Waziri Kivuli wa Fedha, aliyasema hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari juu ya habari iliyoandikwa katika gazeti moja kuhusu wizi wa sh. bilioni 86, unaodaiwa kufanywa na watumishi
wa Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Alisema gazeti hilo (sio Majira), lilitoa taarifa inayodai kuwa, dola za Marekani milioni 54, zimegundulika kuibwa na watumishi waandamizi wa Wizara hiyo na TANESCO, kupitia manunuzi ya mafuta ya kuendesha mtambo wa Umeme wa IPTL.

Aliongeza kuwa, gazeti hilo lilinukuu taarifa ya ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)inayosema kuna kikundi ambacho kazi yake kubwa ni kujifaidisha na mpango wa umeme wa dharura.

“Itakumbukwa kwamba, tangu mwaka 2011, kumekuwa na shinikizo lililotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kuwa zabuni za ununuzi wa mafuta haya na mchakato mzima wa manunuzi yake ufanyiwe uchunguzi wa kina.

“Katika mkutano wa tatu wa Bunge la Kumi April 2011, niliuliza swali bungeni kuhusu kashfa hii ya ununuzi mafuta ya kuendesha mtambo wa IPTL na Aprili 16,2011 nilimwomba Spika airuhusu Kamati ya Nishati na Madini ifanye uchunguzi wa kashfa hii,” alisema Bw. Kabwe.

Aliongeza kuwa, Kamati ya Nishati na Madini chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wake, Bw. January Makamba, ililitaka Bunge kuazimia kufanyika kwa uchunguzi huo katika taarifa yake mwaka 2011 iliyowasilishwa bungeni Aprili 2012.

Alisema Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, Bw. John Mnyika katika hotuba yake ya Bajeti ya Wizara hiyo mwaka 2011, naye alipendekeza ufanyike uchunguzi kuhusu kashfa hiyo lakini
juhudi zote hazikuzaa matunda.

Bw. Kabwe alisema katika kipindi hicho, kiwango kilichokuwa kinahojiwa kuibwa ni sh. bilioni 15 tu, ambapo taarifa ya gazeti
hilo kama walivyonukuu taarifa ya CAG, inaonyesha fedha zilizoibwa ni sh. bilioni 86.

“Zabuni za kununua mafuta ya kuendesha umeme wa dharura zimekuwa zikitolewa bila kufuata utaratibu wa zabuni kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi.

“Hivi sasa kila mwezi Tanzania inatumia dola milioni 70 kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme, fedha hizi zinatoka Hazina na sehemu ndogo kutoka TANESCO,” alisema.

Alisema wakati fedha hizo bilioni 112 zinachomwa kila mwezi kununua mafuta mazito na dizeli ya kuendesha mitambo ya umeme, taarifa za kitaalamu zinaonesha Bwawa la Mtera lina kina cha maji chini ya kiwango kinachotakiwa na uzalishaji umeme ni asilimia 20 tu ya uwezo.

Aliongeza kuwa, kama TANESCO wataendelea kutumia zaidi maji yaliyopo Mtera, mitambo itashindwa kazi na gridi nzima itasimama maana Mtera ndio nguzo kuu ya gridi ya Taifa.

“Hii ni hatari sana kwa uchumi, ulinzi na usalama wa Taifa, gridi ya Taifa ipo hatarini kutokana na kiwango cha maji kilichopo Mtera hivi sasa na kuendelea kupungua kwa kina,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, taarifa ya CAG kuhusu zabuni za manunuzi ya mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura iwekwe wazi pamoja na ile inayoonesha wizi wa sh. bilioni 86.

“Hatua za kisheria zichukuliwe mara moja na bila kuchelewa na Waziri wa Nishati na Madini auleze umma hali halisi ya sekta ya umeme nchini na uzalishaji ukoje, nini hatma ya mitambo ya IPTL, kesi zake na utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuwa kesi za kampuni hii zimalizwe nje ya mahakama,” alisema.

Alisema umefika wakati wa Taifa kuelezwa mpango wa dharura
wa umeme unakwisha lini kwani muda uliotolewa na Bunge
Agosti 2011, tayari umekamilika.

Bw. Kabwe alisema Waziri aeleze hatua gani amechukua baada ya kukabidhiwa taarifa na CAG kuhusu maafisa waandamizi wa Wizara waliohusika na wizi wa fedha za kununua mafuta ya IPTL.

Alimtaka Waziri wa Fedha kuueleza umma ni kiwango gani cha fedha ambazo hazina imetoa kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura kati ya Novemba 2011 hadi Oktoba mwaka 2012, taratibu zote za zabuni kama zilifuatwa na ikiwa hazikufuatwa ni hatua gani PPRA wamechukua dhidi ya waliokiuka sheria ya manunuzi na kuiletea hasara Serikali.


No comments:

Post a Comment