27 November 2012

Nchi 48 zawekwa kundi la nchi maskini duniani


Na Rachel Balama

UMOJA wa Mataifa (UN), umeziweka nchi 48 katika kundi la nchi maskini duniani (LDCs), zikiwemo nchi 33 za Afrika, Asia (9), Pacific (5) na Caribbean (1).

Ripoti ya nchi maskini sana duniani ya mwaka 2012 iliyotolewa na Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD) kutoka Geneva, nchini Uswisi, ilisema idadi ya watu waliohamia Ulaya kutoka nchi maskini sana (LDCs) iliongezeka.

Ongezeko hilo ni kutoka watu milioni 19 mwaka 2000 hadi milioni 27 mwaka 2010, sawa na asilimia 3.3 ya wakazi wote wa nchi hizo.

Kwa mujibu wa ripoti ya nchi maskini sana duniani ya mwaka 2012, iliyotolewa na UNCTAD, ilisema nchi maskini sana duniani zinatoa asilimia moja ya wahamiaji duniani kote.

Imesema wahamiaji wanne kati ya watano kutoka LDCs, wanaishi katika nchi zinazoendelea (Kusini) na mmoja kati wa watano ndiye anaishi kwenye nchi zilizoendelea (Kaskazini).

“Kiwango cha fedha zinazotumwa na raia waliohamia ng’ambo kwenda katika nchi zao, kiliongezeka mara nane kati ya mwaka 1990 na 2011, kutoka dola bilioni 3.5 hadi bilioni 27.

“Mwaka 2011, kiasi cha fedha zilizotumwa kwenda nchini Tanzania kutoka Uingereza zilikuwa dola milioni 4.5, kutoka Canada milioni 3.2 na kutoka Kenya milioni 2.5,” ilisema taarifa hiyo.

Fedha zilizotumwa kwenda LDCs, zilikuwa mara mbili ya thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja (FDI).

Nchi maskini zilizotajwa ni Angola, Benin, Burkina Faso, Burundi, Central African Republic, Chad, Comoros, Congo (DRC), Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau, Lesotho, Liberia, Madagascar na Malawi.

Nyingine ni Mali, Mauritania, Msumbiji, Niger, Rwanda, Sao Tome na Principe, Senegal, Sierra Leone, Somalia, Sudan, Togo, Uganda, Tanzania, Zambia, Afghanistan, Bangladesh, Bhutan, Cambodia, Lao, Myanmar, Nepal, Timor-Leste, Yemen, Caribbean, Haiti,
Kiribati, Samoa, Solomon Islands, Tuvalu na Vanuatu.

5 comments:

 1. tanzania siyo maskini bali uongozi uliojah ufisadi na kutokukusanya kodi ndiyo sababu wananchi wanaonekane ni maskini kwani ni nchi ya pili barani africa kwa viogozi kutumia magari ya kifahari yenye garama kubwa katika uendeshaji ya kwanza ni misri ya pili tanzania yatatu south africa, kwani tuna rasilimali ya kutosha, tuna watu wa kutosha, tuna ardhi ya kutosha na yenye rutuba, ila siasa na viongozi wa kisiasa ndiyo tatizo kubwa

  ReplyDelete
 2. kweli naamini TANZANIA siyo masikini ila serikari yetu imeshindwa kutumia resources vinzuri kama vile madini, ardhi,kilimo. pia kuwa na uongozi legelege umechangia sana, mfano serikari kutoshikiria vyazo vya mapato kama vile mashirika ya usafirishaji wa anga na inchi kavu,viwanda vikubwa.Nashauri serikari kuwa kuleta wawekezaji cyo kuinua uchumi wa inchi na kipato cha wananchi

  ReplyDelete
 3. UKIWA ZUZU HATA MAWAZO YAKO YATADHIHIRISHWA NA YALE UNAOCHACHANGIA TANZANIA NI MASIKINI KUPINDUKIAKA KAMA NI SUALA LA RASILIMALI ASILIA TANZANIA HAIFU DAFU KWA ZAIRE HICHO SIO KIGEZO CHA KUWA NA UCHUMI ULIOENDELEA MBONA BELGIUM HAINA HIZO RASILIMALI ASILIA LAKINI UCHUMI WAKE NI UNAKARIBIA NA UCHUMI WA NCHI ZOTE ZA AFRIKA NI MATUSI JE UNAELEWA HILO ZUZU JAPAN WALA HAINA MADINI YA CHUMA WALA URENIUM LAKINI NI MTENGENEZAJI MASHUHURI WA MELI NA PIA ANAZALISHA NISHATI YA NUCLEA UNAELEWA HILO,SWITZERLAND NI KINCHI KIDOGO SANA HAKUNA MADINI ,MAKAA YA MAWE WALA MADINI YA NUCLEA MBONA UCHUMI WAKE UKO JUU SANA TATIZO WATANZANIA WANAFIKIRI KWA KUTUMIA MAKALIO HAKUNA RASILIMALIWATU HII NDIO BELGIUM,JAPAN NA SWITZERLAND WANAJIVUNIA TUTABAKIA KUBWABWAJI SHIDA HATUELEWI MCHAWI NI NANI KWA TAARIFA YAKO NI SERA CHAFU ZA WORLD BANK NA IMF "UNAWEZA KUSOMA ATHARI ZA UTANDAWAZI KWA BARA LA AFRIKA" LABDA ITAWASAIDIA MAZUZU KUTAFUTA MBINU MBADALA ZA KUPAMBANA NA UTANDAWAZI ,UTANDAZUZU NA UTANDAWIZI SINA UHAKIKA IWAPO MAZUZU WANANIELEWA AKLIYEKUWA NI KIPANGA WA UCHUMI NI NYERERE PEKE YAKE ALIYELAANI WORLD BANK NA IMF AKIWAOMMBA NCHI MASKINI KUUNNDA "SOUTH SOUTH COMMISSION NA MADAI YAKE YA KUUNDWA "NEW INTTERNATIONAL ECONOMIC ORDER " KAFA NA MAWAZO YAKE NI NANI WA KUYAFUFUA KWENYE ULIMWENGU HUU WA MAZUZU NAWAHURUMIA MAZUZU ZIKO DALILI ZA WAZI MUTAWAITA WAZUNGU WAJE WAWATAWLE KWANI MMESHINDWA NCHI ZENU ENDELEENI KUCHEZA BAO,KUVUTA BANGI NA MADAWA YA KULEVYA NA NGONO KWA SANA KWA HERINI

  ReplyDelete
 4. Wanaume wa Tanzania wangefanya kazi kama wanawake wa Tanzania,nchi hiyo ingekuwa nchi tajiri ya kwanza barani la Afrika

  ReplyDelete
 5. Tukiondoa kutoka wanaume wa Tanzania,uvivu,uchoyo,udangaganyifu,rushwa na uvutaji pombe,nchi hii inaingia kwenye orodha ya nchi tajiri duniani

  ReplyDelete