27 November 2012

JK awaapisha Majaji, Katibu Tume ya Sheria


Na Grace Ndossa

RAIS Jakaya Kikwete, jana amewaapisha Majaji wawili wa Mahakama ya Rufaa, mjumbe wa Tume ya Uchaguzi na
Katibu wa kurekebisha sheria.

Majaji waliapishwa katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam  ni pamoja na Profesa Ibrahimu Juma na Profesa Bethuel Mmila,
ambao watakuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.

Pia Rais Kikwete alimwapisha Jaji Mstaafu John Mkwawa, kuwa mjumbe wa Tume ya Uchaguzi na Bi. Winfrida Koroso kuwa
Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria nchini.

Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kuapishwa,
Jaji Mkwawa alisema atajitahidi  kutekeleza majukumu yake
na kuhakikisha malalamiko yote yanayotokea wakati wa
uchaguzi atayafanyia kazi ipasavyo.

Naye Jaji Juma alisema pamoja na changamoto zilizopo katika mahakama nyingi nchini, watajitahidi kuzifanyia kazi na kuhakikisha kesi zilizopo zinaisha mapema.

Hata hivyo, Jaji Juma alisema wananchi wasiwe na utamaduni wa kulalamika badala yake wawe wanafuatilia mienendo ya kesi ndiyo watajua kinachoendelea.

No comments:

Post a Comment