30 November 2012
Maalim Seif aongoza mamia kumzika mke wa Hamad Dar
Na Goodluck Hongo
MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, jana aliongoza mamio ya waombelezaji katika mazishi
ya Kissa Gwalugano Mohamed ambaye ni mke wa Mbunge wa
Wazi, Zanzibar Bw. Hamad Rashid Mohamed.
Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni Pamoja na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Bw. Wiliam Lukuvi, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Ludovick Utouh.
Wengine ni Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda, Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa UDP, Bw. John Cheyo, viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa pamoja na wabunge.
Katika msiba huo, viongozi wa kisiasa waliweka pembeni tofauti zao na kumfariji Bw. Mohamed ambaye chama hicho kiliwahi kumfukuza uanachama.
Mazishi hayo yalifanyika Dar es Salaam jana katika makaburi ya Kisutu, saa kumi jioni.
Akizungumza kwa niaba ya familia, Profesa William Matuja aliwashukuru viongozi wote walioshiriki mazishi hayo kwani wamefarijika sana ingawa wamepata pigo kwa kifo hicho.
Marehemu alizaliwa Oktoba 20,1955 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, alisoma katika Shule ya Msingi Azimio, baadaye Sekondari ya Zanaki jijini Dar es Salaam.
Alisema baadaye alijiunga na masomo ya kompyuta na kuajira THB (iliyokuwa Benki ya Nyumba nchini), lakini alichana kazi na kuamua kujiajiri mwenyewe hadi mauti ilipomkuta.
Alifunga ndoa na Bw. Mohamed mwaka 1984 na walibahatika kupata watoto kati ya hao mmoja wa kiume. Marehemu alikuwa akilalamika kusumbuliwa na mgongo na baada ya kupimwa
iligundulika kuwa na ugonjwa wa mifupa.
Marehemu alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Novemba 27 mwaka huu, baada ya kuzidiwa na kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na kufariki saa tatu usiku.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Innalliahi Wainnaillahi Rajjiuuna - Pole sana Dr Hamad.
ReplyDeleteNawapongeza viongozi wa kisiasa kwa kuonesha umoja - Mungu Ibariki Tanzani!