21 November 2012

CUF wamtaka JK asitishe upimaji ardhi



Na Mwajabu Kigaza, Kigoma

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Prodfesa Ibrahim Lipumba, amemuomba Rais Jakaya Kikwete kusitisha tathmini ya upimaji ardhi inayoendelea mkoani Kigoma kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya nchi kavu katika makazi ya watu.

Prof. Lipumba aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Center katika Manispaa Kigoma Ujiji mkoani hapa na kusisitiza kuwa, haki inapaswa kupatikana kwa
kila mwananchi mwananchi badala ya watu wachache kutaka
kujinufaisha kupitia migogo ya wananchi.

Alisema ujenzi wa bandari hiyo ni muhimu kwa masilahi ya Taifa
na wananchi ila ni muhimu ijengwe katika maeneo ambayo si makazi ya watu hivyo alimuomba Rais Kikwete kuliangalia
suala hilo na kusitisha ujenzi huo mara moja.

“Hili ni jambo la ajabu sana, viongozi wameng'ang'ania kujenga bandari ya nchi kavu katika makazi ya watu licha ya wananchi kuahidi kutoa mashamba kama watalipwa fidia za mazao yao ili
kupisha ujenzi uendelee.

“Inawezekana kuna baadhi ya viongozi tayari wamejaza matumbo yao sasa wanataka wananchi wahame kwa lazima bila eneo ambalo wanataka kujenga bandari hiyo ni makazi ya watu,” alisema.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, aliwataka wakazi wa Mkoa huo kufanya mabadiliko ya dhati ambayo yataleta tija kwa Taifa kwa kuachana na vyama visivyo na dira, sera zisizotekelezeka.

Katika mkutano huo, Prof. Lipumba alikabidhi kadi kwa wanachama wapya 30 ambao walijiunga na chama hicho.

No comments:

Post a Comment