Na Benjamin Masese
SERIKALI imehadharishwa kuimarisha ushirikiano na vyombo vya habari, kutoa taarifa mbalimbali kwa wakati kwani kitendo cha baadhi ya watendaji kushindwa
kutimiza wajibu wao kwa wanaharai kinaweza kujenga chuki miongoni mwa waandishi na Serikali.
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Ananilea Nkya, aliyasema hayo Dar es Salaam jana katia mafunzo ya wanaharakati dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
Alisema kama Serikali itashindwa kuvitumia vizuri vyombo vya habari, inaweza kujenga chuki kati ya Serikali wananchi kwani vyombo hivyo ni tunda la jamii katika kuelimisha na kukosoa.
“Kama Serikali itashindwa kuvitumia vyombo vya habari, ipo dalili ya viongozi kuondolewa madarakani kama ilivyotokea katika nchi zingine za Afrika, Serikali isifanye kazi kwa kutegemea vyombo vya dola kulinda amani na kuwanyima wananchi uhuru wa kueleza wanachoamini.
“Jeshi la Polisi halitaweza kuishinda nguvu ya umma mara itakapochukia na kufanya uamuzi, Serikali inapaswa kujirekebisha ili vyombo vya habari viweze kuripoti mambo ya maendeleo zaidi kupitia radio, televisheni na magazeti,” alisema.
Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha jamii za pembezoni zinatoa taarifa juu ya ukatili wa kijinsia ili Serikali iweze kuchukua hatua zinazostahili kwa wakati husika.
Wanaharakati hao walisema kuwa, Serikali inapaswa kutambua chanzo cha vurugu zinazoendelea duniani hasa katika barani Afrika kuwa ni matokea ya uongozi kushindwa kutambua na kushirikiana na vyomboa vya habari ambavyo vilitumika kueneza sumu na kusababisha umma kuwang'oa madarakani.
No comments:
Post a Comment