26 November 2012

Bashe,Membe mgogoro mzito

Na Mariam Mziwanda

MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Hussein Bashe ameeleza kuwa kwa maslai mapana ya taifa na chama ataendelea kutetea kauli yake na kusimamia aliyoyasema kwenye mkutano mkuu wa chama hicho mjini Dodoma kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  Bernard Membe ni mtu hatari na mnafiki.

Bashe alisema hayo jana jijini Dar es salaam alipozungumza na majira kwa njia ya simu juu ya muafaka wake na waziri huyo aliyeeleza kwenye vyombo vya habari kuwa anataka kumshtaki katika  vikao vya maadili vya chama na mahakamani ili kuthibitisha madai yake.

Alisema kuwa Waziri huyo atambue mtu anayetaka kupambana nae hana historia ya kufanya kitu bila maamuzi ama kwa kutumwa na watu bali anafanya kwa kujiamini na anakila sababu ya kuthibitisha kauli yake mbele ya vyombo vya sheria na atafurahi kama watafikia kwenye vikao vya maadili na mahakamani ili akawadhihirishie umma kuwa kuna mengi maovu dhidi yake na hastahiri kuwa kiongozi wa nchi.

"Kwa muda mrefu Membe amekua akiendesha mapambano dhidi yangu tena kwa kutumia vibaraka wake lakini kwa sasa namshukuru nimemtoa hadaharni na kupitia chama na mahakama anazozitaka nitaendelea kumtoa hadaharani kuwa hana uwezo wa kuwa kiongozi wa dhama hizi hana maono wala hekima ya kuwa kiongozi,"alisema Bashe

Alimtaka Waziri huyo kutambua kuwa anayepambana nae si wale aliozoea kuwatisha kwa maneno anahitaji vitendo kwani histori inamuhukumu kuwa amewaumiza wengi ndani ya chama na nje.

"kwanza aache vitisho na kuimba taarabu atambue anapambana na mtu asiye dhaifu zama zake zimekwisha na mwisho wa kutamba kwake na kuumiza watu pia kumefikia atambue udhaifu wake ni mwingi na nitauwanika wote huko katika vyombo vya sheria"alisema

Bashe alieleza kuwa kiongozi huyo ni mdhaifu wa dhahiri asiyejua hata majukumu yake ndani ya nafasi ya uwaziri hivyo kumpa kazi kubwa Rais Kikwete katika kumsaidia kazi zake kwani hata mgogoro wa mipaka wa Malawi na Tanzania umemshinda huku balozi zetu zikiendelea kuwa na matatizo huko nje.

Alisema mbali na hali hiyo vijana wa Kitanzania wanaendelea kuteseka na kupata shida Ulaya na Marekani huku akimkumbusha kurudisha haki ya Walibya aliyochukua ili kuwaondolie matatizo waliyonayo.

Bashe pia amewapongeza wajumbe wa NEC waliombeba waziri huyo na kusema kuwa bila wao kuwa mbele yake hakuwa na sifa za kupata ujumbe kutokana na uchafu alionao.

Hali hiyo imetokana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe kueleza katika moja ya chombo cha habari jana kuwa yupo tayari kumfikisha Bashe katika chama na mahakama ili aweze kuthibitisha madai yake aliyoyatoa katika vyombo vya habari hivi karibuni mjini Dodoma.

Imeelezwa kuwa Bashe alizungumza na vyombo vya habari mjini Dodoma akimtuhumu Membe kuwa ndiye aliyehusika na vipeperushi vya kumuhujumu Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete kutokuchaguliwa katika nafasi ya Mwenyekiti wa chama ambapo kw aupande w aBbashe alikiri kwlei kuitoa kauli hiyo akiamini mitandao ya kijamii ambayo Membe aliitumia kufikisha taarifa za kumpinga Mwenyekiti kwa wapambe wake.

Waziri Memba alisema kutokana na ushauri na tathimini na wanasheria wake ameamua kumpeleka Bashe katika chama na mahakamani kwani mtu anayeweza kuacha maneno hayo ya Bashe yakapita hewani labda awe amekufa na ili kumjulisha mjumbe huyo Membe ni nani ipo haja ya kutokumwacha hivihivi.

No comments:

Post a Comment