26 November 2012

Waganga wa jadi watakiwa kuacha utapeli Njombe


Na Joseph Mwambije

Njombe

WAGANGA wa jadi Nchini wametakiwa kuacha utapeli na
kuwaambia wateja wao ukweli kama matatizo yao yanatakiwa kutibiwa Hospitali na
kuacha kuwadanganya Wateja wao kuwa wamerogwa wakati homa wanazoumwa ni za
kutibiwa Hospitali.
Wito huo umetolewa na Mganga mmoja  wa Waganga wa jadi Bw. Galus Lihoka wakati
akizungumza na gazeti hili mjini Njombe hivi karibuni kuhusu kuibuka kwa wimbi
la Waganga wa jadi Matapeli ambao wamekuwa wakiipaka matope kazi ya Uganga wa
jadi.


‘Umefika wakati wa watu kuiheshimu shughuli ya utalaamu wa
tiba asilia au uganga wa jadi kama zilivyo shughuli zingine sio mtu akiona hana
kazi ya kufanya anaamua kuwadanganya watu kuwa yeye ni mganga wa jadi na
kuwatapeli watu’,anasema Mtalaamu huyo wa tiba asilia.


Anasema kuwa kutokana
na tatizo la ajira Nchini katika miaka ya hivi karibuni limeibuka wimbi
la Waganga wa jadi Matapeli ambao wamewafa nya Waganga wa jadi au Maarufu kama
Wataalamu wa tiba asilia kutoaminika kwa jamii.


Mtalaamu huyo wa tiba za jadi anayefanyia shughuli zake  Mkoani Njombe na Jijini
Dares salaam anaitaka
jamii kutambua kwamba Uganga wa jadi una miiko yake kama zilivyo shughuli nyingine
na Kwamba na Waganga wa jadi wanaochipukia na kuingia katika shughuli hiyo
kutambua hilo.


Galus Lihoka  amekuwa
akizunguka  Katika Nchi mbalimbali Barani
Afrika kutoa tiba za jadi hasa katika Nchi za Kenya,Msumbiji,Malawi,Uganda na
katika Nchi za Kiarabu.

No comments:

Post a Comment