26 November 2012

Acheni kulima karibu na nguzo za umeme-TANESCO


Na  Patrick Mabula,
Kahama

SHIRIKA la Umeme Taznzania (TANESCO) wilayani Kahama limewataka wananchi kuacha kulima karibu na
nguzo za umeme kwa kuwa zinasababisha kuoza na kuanguka

Kauri hiyo imetolewa kufaatia malalamiko ya wateja juu ya tatizo la kukatikakati
mara kwa mara kwa umeme katika wilaya ya Kahama kitu ambacho kimekuwa kero kwao na
inakwamisha shughuri zao za kijamii za uzalishaji mali.

Wananchi na wateja wa Tanesco wilayani Kahama wamekuwa wakitoa malalamiko yao juu ya
tatizo la katikakati ya umeme ambayo imekuwa ya mda mrefu hali ambayo imekuwa
ikiwakwamisha katika kazi zao za ujasiriamali.

Bw.Omary  Juma mkazi wa mitaa ya Nyasubi mjini Kahama alisema tatizo la kukatika
mara kwa mara kwa umeme na pengine bila taarifa toka Shirika la Umeme ni moja ya
changamoto inayowakabiri kwa mda mrefu katika mambo mbalimbali na imekuwa kikwazo
kwa maendeleo yao.

Alisema tatizo hilo ambalo huwa kubwa sana katika kipindi hiki cha mvua za masika
huwa ni kikwazo sana kwa shughuri za wajasiriamali wanaotegemea  nishati hiyo kwa
kazi zao za kila siku kwenye maisha yao hali waliyomba lifanyiwe juhudi za
kulimaliza .

Meneja wa Tanesco wa Wilaya ya Kahama Bw.Sulle Khabati alisema juzi kuwa tatizo hilo
la kukatika kwa umeme hasa katika kipindi hiki cha mvua za masika limekuwa
likisababishwa na wananchi kulima majaluba ya mpunga kwenye nguzo za umeme.

Bw. Khabati amewataka wananchi kacha mara moja kulima karibu na nguzo za umeme kwa
vile ni chazo kinachofanya kuoza na kuaguka katika kipindi hiki cha masika na
kusababisha nguzo kuaguka na kuleta tatizo la umeme kukatika mara kwa mara lakini
jitihada zinaendelea kufanyika kukabiliana na kero hiyo.

No comments:

Post a Comment