07 September 2012
Zungu atoa vifaa vya michezo Jangwani
Na Anna Titus
MBUNGE wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu jana ametoa vifaa vya michezo kata ya Jangwani,Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kukarabati viwanja vya michezo katika kata hiyo.
Akizungumza jana Dar es Salaam jana wakati akikabidhi vifaa hivyo Zungu alisema ni mwaka wa sita sasa timu zote za jimbo hilo anazisaidia japo si kwa 100% ambapo ameahidi kuwa mwaka huu atahakikisha anazisaidia timu zote katika kata hiyo.
Aliongeza kuwa kwa sasa wanafanya bonanza la matumaini pia kutakuwa na kikombe maalumu kwa ajili ya mashindano, lengo likiwa ni kuboresha timu hizo za Ilala na kuleta changamoto na ushindani mkubwa.
"Tayari kikombe tumeshanunua cha sh.milioni moja na nusu kwa ajili ya timu zote za Ilala ambazo zitashindania.
"Tulitoa ahadi ya kuboresha viwanja vya michezo na sasa tumeanza na tunaendelea, ili kuhakikisha tunasaidia vijana wote wenye vipaji na pia iwe changamoto kwa viongozi wengine, " alisema Zungu
Katika risala iliyosomwa Kocha Msaidizi wa timu ya Bom Bom, Uwesu Ahmad alimpongeza Mbunge huyo kwa kuwapatia mipira na nyavu vyote vikiwa vimegharimu sh. milioni moja ikiwa na kuwakarabatia uwanja.
Kocha huyo alisema timu yake inatarajiwa kushiriki Ligi ya TFF pamoja na timuya Congo Shooting hivyo walikuwa wanahitaji msaada wa jezi, nauli pamoja na posho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment