24 September 2012
Watoa huduma za kisheria waonywa
Na Pendo Mtibuche,
Dodoma
WATOA huduma za kisheria kwa wananchi hapa nchini wameonywa kutojihusisha na ushabiki wa kisiasa pindi wanapotoa huduma hiyo.
Angalizo hilo lilitolewa jana na Meneja wa Mfuko wa Legal Services Facility (LSF),Bw
Kees Groenendijk wakati akizungumza na watoa huduma hao wa kisheria wa mikoa yote
Tanzania Bara.
Menaja huyo alisema kuwa hivi sasa kumeibuka baadhi ya watoa huduma hao kuanza
kujiingiza katika vitendo vinavyokiuka maadili ya kazi yao.
Alisema kuwa pindi wanapokwenda kutoa huduma za kisheria kwa wananchi wajiepushe na
uvaaji hata wa sare za chama chochote, lakini pia hata katika ofisi zao kusiwe na
bendera ya chama chochote.
"Hivi sasa kuna baadhi ya watoa huduma ambao wanawatoza fedha wananchi wanaokwenda kwao kupata huduma jambo ambalo alisema kuwa si sahihi kwa kuwa watoa huduma hao wanapata fedha za ufadhili katika kuendesha kazi zao hivyo hawapaswi kuwatoza wananchi fedha,"alisema
Hata hivyo mbali na kukemea masua la ushabiki wa kisiasa lakini pia aliwaonya watoa
huduma hao kujiepusha na utoaji wa huduma mwa kuangalia kabila au udini na kusema kuwa kufanya hivyo wanakiuka miiko ya kazi yao.
Hali kadhalika alisema kuwa LSF ipo kwa ajili ya kutafuta fedha katika nchi mbalimbali ambazo zitasaidia wananchi wengi kupata haki zao kupitia wasaididzi hao wa kisheria.
"Hivi sasa nahangaika kutafuta fedha dora milioni 300 katika maendeo mbalimbali nje ya nchi fedha ambazo lengo lake nataka zikipatikana zije kusaidia wananwake wa hapa nchini kupata haki zao,"alisema.
Mbali na hayo pia alisema kuwa hapa nchini bado kuna tatizo kubwa la upatikanaji wa takwimu sahihi hasa kwa upande wa sekta ya sheria jambo ambalo alisema kuwa huenda hata taifa likashindwa kuwa natakwimu sahihi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment