24 September 2012
Milioni 200 Kinondoni zitumike kuwezesha wanawake,vijana-Mnyika
Na Rose Itono
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, kuhakikisha kinatumia fedha kiasi cha milioni 200 zilizotengwa wakati wa bajeti ya 2012/2013 kwa ajili ya kuviwezesha vikundi vya wanawake na vijana ili viweze kujiajiri.
Bw. Mnyika aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati wa ziara ya kichama na baadaye kuzinduzi matawi,misingi na ofisi ya Chama Kata ya Mabibo Dar es Salaam.
Mbunge huyo alisema kuwa serikali imetenga fedha hizo ili kuviwezesha vikundi hivyo kupata mikopo.
Bw. Mnyika alisema CHADEMA kimewezesha kuhamasisha serikali ili kuongeza fedha kwa ajili ya vikundi hivyo kutoka kiasi cha Sh.milioni 20 hadi kufikia kiasi cha Sh. milioni 200.
Mbali na hilo mbunge huyo aliwataka viongozi kuacha kugeuza misingi na matawi wa Chama hicho kuwa vijiwe na badala yake kuhakikisha wanashughulikia kero za wananchi.
"Viongozi msigeuze matawi kama sehemu ya kupigia majungu bali, bali tumieni kwa ajili ya kutatua kero za wananchi ili kuleta maendeleo kwa jamii",alisema.
Aliongeza kwa kuwataka viongozi wa matawi kujenga ushirikiano na viongozi wengine katika kuleta maendeleo bila kujali itikadi za kichama.
Hata hivyo Bw. Mnyika alizindua matawi mawili na misingi minne katika mitaa ya Jitegemee na Mabibo farasi iliyopo Jijini.
Alisema CHADEMA imekuwa ikizindua misingi katika kata za jimbo lake ili kujenga siasa safi kuanzia ngazi ya chini mpaka Taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment