05 September 2012
UVCCM: Tutasimama imara kulinda amani iliyopo
Na Stella Shoo, Morogoro
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, umesema upo tayari kulinda amani iliyopo nchini kwa ghrama yoyote nma kuvitaaka vyama vya upinzani kunadi sera zao badala ya kuvunja sheria za nchi.
Akizungumza na gazeti hili kwa niaba ya umoja huo, Katibu wa CCM wilayani hapa, Bw. Sambo Dodo, alisema chama hicho hakifurahishwi na vitendo vya kuvuruga amani iliyopo vinavyofanywa na baadhi ya vyama vya upinzani nchini.
“Kila chama cha siasa kina haki ya kunadi itikadi ya chama chao lakini amani ni muhimu sana, viongozi wa siasa ni vyema wakazingatia sheria za nchi ili kuepusha vurugu,” alisema.
Bw. Dodo aliongeza kuwa, baadhi ya vyama vya hivyo vimekuwa vikitoa lugha ya matusi jukwaani pamoja na kejeli kwa Rais Jakaya Kikwete na viongozi wengine hivyo kama tabia hiyo haitakoma, wananchi watakosa imani na vyama vyao.
“Mimi binafsi pamoja na UVCCM wilaayani hapa, tunampongeza Rais Kikwete kwa uvumilivu alionao na umakini katika siasa, tupo pamoja naye kuwatetea wananchi na kuilinda nchi,” alisema.
Alivitaka vyombo vya dola kuvichukulia hatua vyama vya siasa ambavyo vinatumia majukwaa yao vibaya kwa kutoa matusi na kejeli dhidi ya kiongozi wa nchi na viongozi wengine wa Serikali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment