20 September 2012

...TBL kuzukabidhiwa Marcopolo zao leo


Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia Bia ya Kilimanjaro Premium lager, hatimaye inatarajia kukabidhi mabasi mapya ya kisasa kwa timu za Simba na Yanga kesho asubuhi.

Akizungumza Dar es Salaam jana Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema maandalizi yote yamekamilika na makabidhiano hayo yatafanyika katika viwanja vya ofisi za TBL Ilala.

“Zaidi ya wageni 100 wamealikwa kwenye hafla hii itakayofanyika Ijumaa hapa TBL na kati ya hawa wageni, kutakuwa na baadhi ya mashabiki wa timu hizi mbili kwa hivyo tunatarajia makabidhiano ya aina yake,” alisema Kavishe.

Kavishe alisema baada ya makabidhiano, kila timu itaondoka na basi lake ikiwa na wachezaji pamoja na mashabiki na kupita katika matawi yao kwa msafara maalumu, utakaoambatana na burudani mbalimbali.

Alisema msafara wa Simba ukiondoka TBL, utakwendatawi la Vuvuzela lililopo Makao Makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, kisha tawi la Mpira Pesa Magomeni, Ubungo katika kituo cha mabasi na Tawi la Wailes Temeke.

Kavishe alisema msafara wa Yanga nao ukiondoka TBL utakwenda tawi la Ubungo katika kituo cha mabasi, tawi la Manzese, Lango la Jiji Magomeni, Buguruni, Mwembe Yanga, Mtoni kwa Aziz Ali, Mkombozi na kumalizia makao makuu Jangwani, Kariakoo.

"Tunawaomba mashabiki wa timu hizi mbili wajitokeze kwa wingi katika mawati yao, ili wajionee mabasi haya mapya ambayo ni ya kisasa na pia wapate fursa ya kukutana na wachezaji wa timu zao," alisema Kavishe.

No comments:

Post a Comment