20 September 2012

Mashujaa, Komedy Orijino kupamba Redd's Miss Temeke



Na Mwandishi Wetu

BENDI ya muziki wa dansi ya Mashujaa Musica, inatarajia kunogesha mashindano ya Redds Redd's Miss Temeke 2012, yatakayofanyika kesho katika Ukumbi wa PTA, Dar es Salaam


Akizungumza Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa BMP Promotions, Benny Kisaka alisema Mashujaa inayoundwa na wanamuziki nguli imeahidi kutoa burudani ya nguvu ili kuwapa uhondo wadau wa urembo watakaofika ukumbini hapo.

Alisema licha ya bendi hiyo kuahidi kutoa burudani ya nguvu, pia kundi la Ze Comedy Original na Steve Nyerere watatoa vionjo katika mashindano hayo.

Alisema warembo wa Miss Temeke wamekuwa wakijifua kwa wiki tatu chini ya ukufunzi wa Leyla Bhanji, ambaye amekuwa akisaidiwa na warembo wa miaka ya nyuma wa Miss Temeke akiwemo, Regina Mosha (2002) na Hawa Ismail (2003) na Cynthia Kinasha wa THT katika shoo.

Alisema washiriki watakaopanda jukwaani kesho ni 15 kutoka katika vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe.

Mbali ya Redd's, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na City Sports Lounge, Jambo Leo, Mariedo Boutique, Global Publishers, Dodoma Wine, Push Mobile,  Mariedo Boutique, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders, Fredito Entertainment, katejoshy.blogsport.com na 88.4 Cloud's FM.

Benny Kisaka
Mkurugenzi BMP Promotions

No comments:

Post a Comment