05 September 2012

Miss Talent Kinondoni, Ilala Ijumaa


Na Anna Titus

MICHUANO ya kuwania taji la Miss Talent Tourism 2012 katika Wilaya za Kinondoni na Ilala, yanatarajia kufanyika keshokutwa.

Akizungumza Dar es Salaam juzi mratibu wa mashindano hayo, Gabriel  Benedict alisema mnyange atakayetwaa taji hilo atajinyakulia sh. 200,000.


Alisema mashindano hayo yatafanyika katika Ukumbi wa hoteli ya Lamada, huku yakinogeshwa na burudani kutoka katika kundi la Jahazi Morden Taarabu chini ya Mzee Yusuf.

Mratibu huyo alisema mashindano hayo yatashirikisha wanyange 24, ambapo 12 watatoka Kinondoni na wengine 12 wanatokea Ilala.

"Kila kitu kimekamilika kuhusiana na mchuano huo, tunatarajia kutakuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na kila mshiriki kujipanga kikamilifu," alisema mratibu huyo.

Alisema wameamua kuunganisha wilaya hizo kufanya mashindano yake siku moja kwa kuwa tarehe zao zinakaribiana, tofauti na Temeke.

Benedict alisema kiingilio katika mashindano hayo, kitakuwa sh. 20,000 kwa viti maalumu na sh. 10,000 kwa viti vya kawaida.

Mratibu huyo alisema baada ya kufanyika Miss Talent, mashindano ya kuwasaka washindi wa Miss Toursm 2012 kwa wilaya hizo yatafanyika Septemba 14, mwaka huu.

Alisema mashindano hayo yamedhaminiwa na kituo cha Redio Times, Dar City College, Lamada Hotel, Easy Media, Pandisha Import, Zizou Fashion, T-Moto Bank na Daja Saloon.


No comments:

Post a Comment