24 September 2012

Anusurika kufa kwa wivu wa mapenzi


Thureya Dabas na Leah Daudi

RAIS wa Philipino Bi. Romina Maiga (28), mkazi wa Kipunguni, Dar es Salaam, amenusurika kufa baada ya kumeza vidonge kwa lengo la kutaka kujiua kutokana na wivu wa mapenzi.


Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marietha Komba, alisema tukio hilo limetokea juzi usiku ambapo Bi. Maiga alikunywa vidonge ambavyo havijahahamika vya aina gani wala idadi.

Alisema Bi. Maiga ambaye hivi sasa amelazwa katika Hospitali ya Amana, Ilala, alimtuhumu mumewe Bw. Peter Maiga (32), kuwa na wanawake wengine ambapo upelelezi wa tukio hilo unaendelea.

Katika tukio jingine, Kamanda Komba alisema mkazi wa Buguruni James Rubisha (28), amekutwa amejinyonga nyumbani kwake kwa kutumia shuka na kuacha ujumbe ulioeleza historia yake.

Tukio hilo limetokea mchana ambapo siku nne kabla ya kifo hicho, Rubisha aliugua ugonjwa wa malaria na mwili wake imehifadhiwa katika Hospitali ya Amana.

Wakati huo huo, mtoto Yahaya Hatibu (5), mkazi wa Segerea chama, alitumbukia katika kisima cha maji kilichopo jirani na nyumba kwao na kufariki dunia.


Kamada Komba alisema mtoto huyo alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitali binafsi iliyopo Tabata.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa, marehemu na mdogo wake waliondoka nyumbani kimakosa kwani baba yao aliwataka baada ya kurudi Madrasa, wasitoke nje ya nyumbani kwao. Mwili wake umuhifadhiwa Hospitali ya Amana.

1 comment:

  1. nawezaji kupata gazeti lenu kama hard copy kwa kipindi ambacho si rasmi yaani gazeti lilipita kwa mfano mwezi mmoja hata na zaidi?

    ReplyDelete