10 September 2012

Mgosi amvimbisha kichwa Kilinda



Na Amina Athumani

KOCHA wa timu ya JKT Ruvu, Charles Kilinga amesema kujiunga kwa mchezaji, Musa Hasan 'Mgosi' kwenye kikosi chake kumekifanya kikwe na   nguvu kubwa katika mashindano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayotarajia kuanza Septemba 15, mwaka huu.

Mgosi alijiunga na timu hiyo baada ya mkataba wake na DC Motema Pemba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kumalizika na kuamua kuja kumalizia soka lake katika timu hiyo.

Akizungumza na gazeti hili jana Dar es Salaam, Kilinga alisema kikosi chake kipo tayari kushiriki mashindano hayo i ambayo ndiyo mashindano makubwa kwa soka kwa Tanzania.

Alisema kikosi chake kimeimarika zaidi baada ya kukifanyia marekebisho kutokana na mapungufu aliyoyaona katika kligi ndogo ya sita teule iliyofanyika hivi karibuni na kuzikutanisha timu za Jeshi.

''Kwa sasa naweza kusema kikosi changu kipo tayari kimashindano, nimekipika na kimeiva, hivyo mashabiki wasubiri mambo makubwa kutokana na ukweli kwamba mwaka huu tumejiandaa vya kutosha,''alisema Kilinga.

Alisema kutokana na hali hiyo atahakikisha mechi tano za awali katika ligi hiyo waanafanya vema ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment