26 September 2012

Maofisa 49 JWTZ wapanda vyeo



Na Stella Aron

AMIRI Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete, amewapandisha vyeo Maofisa 49 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kuanzia Septemba 21 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana kwa vyombo vya habari kutoka Makao Makuu ya JWTZ, ilisema Meja Jenerali Samuel Ndomba amepanda kuwa Luteni Jenerali.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kuwavisha cheo kipya Maofisa hao, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange, alisema Rais amemteua Luteni Jenerali Ndomba kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ kushika nafasi iliyoachwa wazi Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo, ambaye amestaafu utumishi jeshini.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa, kabla ya uteuzi huo Luteni Jenerali Ndomba alikuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Wengine waliopandishwa cheo ni Brigedia Jenerali Rafael Muhuga kuwa Meja Jenerali na kuwa Mkuu mpya wa JKT, nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Ndomba.

Kabla ya uteulizi huo, Meja Jenerali Muhuga alikuwa Mkuu wa Utawala wa jeshi hilo.

Makamanda wengine waliopandishwa vyeo kutoka Brigedia Jenerali kuwa Meja Jenerali miongoni mwao wamo Maofisa Wakuu wa kike, Meja Jenerali Grace Mwakipunda kuwa Kaimu Mkuu wa Utumishi Jeshi na Meja Jenerali Lilian Kingazi ambaye ni Mkurugenzi wa Utumishi Jeshini.

Wengine ni Meja Jenenali, Farah Mohamed, Kevin Msemwa, Patrick Mlowezi, Charles Jitenga, Charles Mzanila, Daniel Igoti, Vicent Mritaba, Ipanda Ipanda, Adam Mwabulanga, Ezekiel Kyunga, Projest Rwegasira na Juma Kapwani.

Taarifa hiyo iliongeza Jenerali Mwamunyange, aliwavalisha vyeo vipya makamanda 33 waliokuwa na Cheo cha Kanali kuwa Brigedia Jenerali ambao ni Pellegrin Mrope, Ryakitimbo Ryakitimbo, Mimy Abdallah, John Chacha, Ezira Ndimbwambo, Augostino Gailanga, Gadence Milanzi, Masumbuko Mndeme, Daniel Laswai na Sarah Rwambali.

Wengine ni Mathew Sukambi, Narcis Lubamba, Mwapipo Kyalaliko, Mateka, Jairo Mwaseba, Abdullah Mwenjudi, Cosmas Kayombo, Honoratus Lyamba, Ramadhani Kimweri Nicodem Mwangela, Abbas Mnyani na Rukyaa.

Makamanda wengine ni Elias Athanas, Fabiani Mangore, George Mashamba, Zoma Kongo, Harison Masebo, Paul Masao, Clemence kahama, Jacob Mohamed, Mbazi Msuya, Alfred Kapinga na George Ingrim.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya makamanda wenzake wa ngazi za juu, Luteni Jenerali Ndomba, alisema watayatekeleza majukumu waliyopewa kwa ufanisi mkubwa.

Alimwomba Jenerali Mwamunyange kufikisha shukurani zao kwa Rais Kikwete kutokana na imani aliyonayo kwao kwa kuwapandisha vyeo na kuwapa madaraka mapya.

No comments:

Post a Comment