24 September 2012

Makanda 100 waandamana kuwaondoa vigogo CCM



Na Daud Magesa, Sengerema

ZAIDI ya makada 100 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  wakiwemo viongozi wa Mashina na Matawi, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, wamefanya maandamano ya amani kushinikiza baadhi ya viongozi wa Kamati ya Siasa wilayani hapa kujiuzulu.

Lengo la maandamano hayo ambayo yamefanyika jana ni kuwataka viongozi wa kamati hiyo kutogombea uongozi wowote ndani ya chama hicho kwa madai ya kushindwa kuwajibika na kusimmaia rasilimali za chama ukiwemo ujenzi wa Ofisi ya CCM Wilaya.

Maandamano hayo yalianza kimya kimya ambapo kila mwanachama alikwenda mwenyewe katika eneo walilopanga kukutana na kutembea hadi katika eneo la ujenzo wa ofisi hiyo.

Makada hao walipokewa na kada mwenzao, Kibisa Muyoba, wakiwa na mabango, mkataba wa ujenzi wa jengo hilo na kuazimia malalamiko yao yafikishwe kwa uongoz wa CCM Mkoa kwa maandishi wakidai uongozi wa Wilaya hauwezi kuwasikiliza kutokana na tuhuma ubadhirifu wa fedha zinazowakabili.

Taarifa ya madai hayo ilisomwa na Bw. John Dickson, alisema uvumilivu wao wa kuburuzwa na kufumbia macho uchafu unaodfanyika ndani ya chama hicho umefika mwisho.

'”Hatuwezi kukaa kimya wakati tunaona rasilimali za chama zinahujumiwa, lazima tuzisimamie bila kurudi nyuma, katika hili hatuna huruma hadi kieleweke na watuhumiwa wang'oke,” alisema.
Katibu wa CCM wilayani hapa, Bi. Magreth Ndwete, alipoulizwa kuhusu sakata hilo alikiri kulifahamu na kudai tayari Mkandarasi wa mradi huo Mahenda Sokoni, aliitwa Agosti 31 mwaka huu na Kamati ya Siasa Wilaya.

“Mkandarasi amepewa siku 45 awe amekamilisha ujenzi huo  ifikapo Oktoba 15 mwaka huu na kukabidhi vinginevyo atawajibishwa na kushtakiwa,” alisema.

Alisema hakuna ubadhirifu wowote katika mradi huo ambao thamani yake ni sh. milioni 22.

No comments:

Post a Comment