11 September 2012

Kidonge cha kutibu Malaria chazinduliwa



Na Jesca Kileo

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, jana imezindua kidonge cha kutibu ugonjwa wa Malaria ambacho kitakuwa kikisambazwa na Bohari Kuu ya dawa nchini (MSD).

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, baada ya uzinduzi huo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi, alisema lengo ni kuutokomeza ugonjwa huo.

Alisema ugonjwa huo ni tishio kwa Taifa ambapo utafiti wa kina unaonesha kuwa, watu 80,000 wanapoteza maisha kila mwaka.

Dkt. Mwinyi aliongeza kuwa, Tanzania inatumia kiasi kikubwa cha fedha kupambana na ugonjwa huo ili kununulia dawa za kumeza, kupuliza na vyandarua vya kuzuia mbu.

“Hadi sasa Taifa limefanikiwa kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa huu asilimia 60 kwa watoto kutokana na juhudi zilizofanywa na Wizara hii,” alisema Dkt. Mwinyi.

No comments:

Post a Comment