24 September 2012
Kamera,kompyuta kufungwa kuthibiti madereva wazembe
Na Heri Shaaban
SERIKALI imesema kuwa inamkakati wa mpango wa kufunga kamera na kompyuta Mkoani humo,zitakazokuwa zikiorodhesha madereva wanaosababisha ajali za kizembe pamoja na kuvunja sheria.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana, Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Bw.Raymond Mushi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Bw.Said Mecky Sadiki katika madhimisho ya kilele cha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.
Bw.Mushi alisema kuwa mpango huo ukikamilika Kamati ya Usalama mkoa watakuwa na mtambo maalum wa kompyuta utakaokuwa ukiangalia madereva wazembe pamoja wavunjaji sheria ili waweze kuwachukulia hatua.
"Kamati ya Usalama mkoa imepanga mpango huo kwa ajili ya kupunguza ajali za madereva wetu ambao ni wakiukwaji wakubwa wa sheria waweze kuchukulia hatua iwe njia moja wapo ya kupunguza ajali hizo,"alisema.
Alisema kuwa sasa hivi kutokana na kukuwa kwa teknolojia ya mawasiliano kuna magari mengine yanatumia kumpyuta bila dereva na hayasababishi ajali hivyo kuwaomba madereva wawe makini.
Pia alisema kuwa mkoa unachangamoto nyingi zinazoikabili jiji zikiwemo idadi kubwa ya magari na watu pamoja na maradhi yasiyo na tiba kama UKIMWI.
Aliziagiza Mamlaka husika kuweka utaratibu maalum katika maeneo yao ili kuwapa vibali vya kufanya kazi madereva wa pikipiki katika Manispaa tatu za jiji ambao watamaliza mafunzo endelevu ya bodaboda.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa kamati Usalama mkoa huo,Bw.Jeremih Makorere alisema kuwa mkoa huo katika wiki ya usalama barabarani wameweza kutoa elimu maeneo mbalimbali ya jiji kwa madereva wa bodaboda kwa madereva 1400.
Pia katika kutoa elimu hiyo kwa madereva wa pikipiki wameweza kuchangia mpango wa damu salama uniti 162, na magari yaliyokaguliwa 13,286 yalikabidhiwa stickers magari 13,084 baada kuonekana mazima na mabovu 202yalitakiwa yakatengenezwe alafu yakaguliwe upya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment