05 September 2012
JK kukutana na wakuu wa nchi za SADC leo
Na Rehema Maigala
RAIS Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika), ameitisha mkutano wa dharura ambapo utashirikisha wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Nchi za Kuisni mwa Afrika (SADC), ambao umepangwa kufanyika leo.
Mkutano huo umelenga kuzungumzia mgogoro uliopo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilisema mkutano huo utajumuisha wajumbe wa asasi hiyo kwa ajili ya kuzungumzia mgogoro huo.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa, mkutano huo utakuwa wa siku moja na utafanyika Dar es Salaam ambapo nchi zitakazohudhuria ni pamoja na Msumbiji ambayo ndiyo Mwenyekiti wa sasa (SADC).
Nchi nyingine ni Afrika Kusini ambaye alikuwa Mwenyekiti wa asasi hiyo kabla ya Tanzania na Namibia ambao ni Makamu Mwenyekiti wa Troika. Wakuu wa nchi zote tayari wamewasili nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment