06 September 2012
EBBS yatoa fursa kwa wapenzi wa muziki
Na Mwandishi Wetu
WAPENZI wa muziki wa kizazi kipya wanaotaka kujiunga na washindi 20 wa mashindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS), watakaoingia kambini hivi karibuni wametakiwa kutumia fursa pekee iliyobakia itakayowawezesha kutimiza ndoto zao.
Fursa hiyo ni kufanya usaili kwa njia ya simu, ambayo inatoa fursa kwa ambao hawakupata nafasi ya kuonesha vipaji vyao katika usaili pamoja na ambao walionesha vipaji vyao, lakini hawakuchaguliwa wakati wa usaili wa mashindano hayo.
Akizungumzia njia hiyo Jaji Mkuu wa EBSS 2012, Ritha Paulsen alisema Septemba 13 ndiyo itakuwa mwisho wa kutumika kwa njia hiyo ya kutafutia vipaji hivyo, amewataka watu kuitumia njia hiyo mapema kusaka vipaji.
“Utaratibu huu wa kufanya usaili kwa njia ya simu uliwekwa maalumu kwa watu wanaotaka kujaribu bahati zao tena, baada ya kushindwa kupita kwenye usaili mara ya kwanza, au wale ambao hawakupata kabisa fursa ya kuwaona majaji.
"Aidha kwa sababu hawakuwafikia mikoani kwao, au hawakuweza kufika kwenye usaili kwa sababu zozote zile,” alisema Rita.
Alisema vijana wanaotaka kushiriki usaili kwa njia ya simu wanaweza kupiga namba 090155100, ambapo watapatiwa maelekezo ya namna ya kurekodi sauti zao na kisha zitasikilizwa na majaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment