24 September 2012

CHAMAMATA yakabiliwa changamoto nyingi




Na Heri Shaaban

CHAMA cha Madereva wa Malori Tanzania (CHAMAMATA) kinakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiutendaji ndani ya chama hicho, sababu zinazochangia kukwamisha maendeleo ya chama katika kutekeleza majukumu yake.


Akizungunza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CHAMAMATA, Bw. Clement Masanja, alisema baadhi ya changamoto hizo zinazokwamisha maendeleo ya chama ni ukosefu wa mikataba baina ya madereva na waajiri wao na kutokuwepo kwa mishahara ya kutosha.

"Wajiri wanashindwa kuwapa mikataba ya kudumu madereva wao  wanaosafiri na magari makubwa, pia katika mpaka wa Tunduma magari yanashindwa kuvuka kwa muda unaotakiwa, hivyo kulazimika kukaa katika foleni zaidi ya siku kumi,"alisema, Bw.Masanja.

Changamoto zingine Wizara ya Ujenzi kuwatoza faini wakati wakiegesha gari kwa muda barabarani jambo ambalo wameitaka wizara hiyo kubadilisha sheria hiyo kwanza.

Alisema kutokana na changamoto hizo chama hicho Septemba 23, mwaka huu, kinafanya mkutano wake mkuu wa wanachama wote madereva Tanzania utakaofanyika Tunduma kujadili changamoto ndani ya chama kwa kipindi cha miezi mitatu.

Pia alisema mbali na kujadili changamoto ndani ya chama hicho, pia wanachama wametakiwa kufika ili kuunda kamati ya maadili ya viongozi, kuunda kamati yamarekebisho ya katiba, kuchagua viongozi wa Kanda ya Ziwa, Kanda Kusini na Dar es Salaam.

Aliagiza wanachama kushiriki mkutano huo ili kama wana kero ziweze kujadiliwa na mkutano mkuu ambapo kauli mbiu mwaka huu ni "Kwa Pamoja Tunaweza"


No comments:

Post a Comment