24 September 2012

Wananchi kupewa elimu kulinda malimilki


Darlin Said

TUME ya Ushindani Tanzania(FCC) na Kampuni ya programu ya Kompyuta Microsoft wamekubaliana kutoa elimu bure kwa jamii juu ya umuhimu wa kulinda haki za malimilki ili kusaidia ukuaji wa sekta ya programu za kompyuta ambayo itasaidia kuchochea ukuaji wa uchumi hapa nchini.
 .

Uamuzi huo umetolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa FCC  Bw.Allan Mlulla wakati akisaini mkataba na Kampuni hiyo Dar es Salaam.

Bw. Mlulla alisema kupitia elimu hiyo kampuni hizo mbili wataweza kupambana na uharamia na vitendo vya kutengeneza  bidhaa bandia za programu za kompyuta ambazo sio nzuri.

Bw. Mlulla alisema mbali na elimu hiyo pia watasaidia kuwalinda wateja kufahamu bidhaa halali na bidhaa bandia ili kuweza kudhibiti uingiaji wa mali bandia katika program za kompyuta.

Naye Meneja wa Kampuni ya Microsoft Afrika Mashariki na Kusini alisema mashirika hayo mawili kwa pamoja wataendeleza programu ya Kompyuta na kampeni za kuelimisha kwa kutoa taarifa kwa wakala na umma kuhusu hatari na adhabu zinazohusishwa na ukiukwaji wa haki milki wa program na alama ya biashara.

“Kwa kufanya hivyo itasaidia  kuongezeka kwa ununuzi wa Programu halisi ambazo zitasaidia kupunguza kuzagaa kwa bidhaa bandia feki, “alisema

Hii ni mara ya kwanza Tume ya Ushindani kwa kushirikiana na Kampuni ya program kama Microsoft kushirikiana katika kupambana na uharamia ambao unaua soko la Afrika,ambapo wateja wengi hudanganywa kwa kununua program haramia na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu.

No comments:

Post a Comment