19 September 2012

Bweni la wanafunzi lateketea moto


 Na Bryceson Mathias

WANAFUNZI 48 wa Shule ya Msingi Chimala Misheni iliyopo mjini Mbeya, wamenusurika kufa baada ya bweni walilokuwa wakilala kuteketea kwa moto, nguo zao na vifaa vingine.

Tukio hilo limetokea juzi jioni ikiwa ni mara ya pili kwa mabweni ya shule hiyo kuungua ambapo hivi karibuni, bweni la wasichana wa sekondari nalo liliteketea kwa moto pamoja na vifaa vyao.

Akizungumza na mwandishi wetu katika eneo la tukio, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Venance Mwanjelile, alisema wakati
moto huo unatokea, wasaidizi wa watoto hao (wahudumu), hawakuwepo katika eneo la shule.

“Watoto tumewahifadhi katika jengo jingine wakiwa kama walivyo,  mtoto mmoja alikuwa anachezea kiberiti na mhudumu wetu wa watoto hakuwepo,” alisema Bw. Mwanjelile.

Mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake anasoma shuleni hapo (jina linahifadhiwa), alisema baadhi ya wazazi wanafikiria kuwahamisha watoto wao wakiamini usalama wao shuleni hapo ni mdogo.

“Naiomba Menejimenti ya shule itafute kiini cha tukio hili kwani imani ya wazazi, watoto wao hawapo katika eneo salama kwa malezi na masomo,” alisema.

No comments:

Post a Comment