11 September 2012

Askofu: Vyama vya siasa nchini viheshimu sheria



Na Heri Shaaban

VYAMA vya siasa nchini vimetakiwa kuheshimu sheria za nchi ili kukomesha mauaji ya watu wasio na hatia sambamba na kufanya maombi ili kulinda amani iliyopo nchini.

Askofu wa Kanisa la Hayo yalisemwa, Dar es Salaam jana, Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Jimbo la Mashariki, Lawrence Kametta, katika ibada ya kuwasimika viongozi wa makanisa hayo iliyofanyika Buguruni Sokoni.

Alisema kila mwanadamu kama ataheshimu sheria za nchi na kumtanguliza Mungu katika Misha yake, atakuwa amesaidia kukomesha mauaji yanayojirudia mara kwa mara.

“Nawaomba Watanzania tuombee nchi yetu ili damu isimwagike, tukomeshe migomo ya mara kwa mara, tumuombee Rais wetu na wasaidizi wake waweze kumshauri vizuri,” alisema.

Aliwataka Mawaziri na wabunge kufanya kazi zao kwa uwazi na ukweli sambamba na kuviomba vyama vya siasa vitekeleze majukumu ya kuwatumikia wapiga kura wao.

Katika hatua nyingine, Askofu Kamatta aliwataka wachungaji kuwa viongozi wazuri na kuhakikisha waumini wao wanamrudia Mungu na kuzingatia mafundisho yake kwa vitendo.

“Wachungaji wajibikeni kuliombea kanisa liweze kukaa katika nafasi yake kwa kufuata miongozo mliyojiwekea na waumini washirikiane na viongozi wa kanisa ili kuhakikisha nane la Mungu linabadilisha maisha ya Watanzania,” alisema.


No comments:

Post a Comment