Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bi. Badra Masoud (kushoto), akionesha moja ya mita za umeme wa LUKU za shirika hilo, zilizokamatwa pamoja na vifaa vingine kwenye nyumba namba 182 Mwananyamala A, wakati wa operesheni ya kukamata wezi wa umeme, Dar es Salaam jana. Kulia ni mtuhumiwa aliyekamatwa na vifaa hivyo, Bw. Said Ibrahim. (Picha na Charles Lucas)
Ndugu mhariri taarifa hii ya wizi wa umeme inakanganya kwani mtuhumiwa anasema kampuni yake imesajiliwa kusambaza umeme kama contractor
ReplyDeleteKweli katika nchi zilizoendelea kama Marekani mbali na kuwepo na kampuni kubwa kama PEPCO ambayo ni sawa na TANESCO zipo kampuni ndogo ndogo ambazo zimesajiliwa na kushirikiana na PEPCO katika kusambaza na kuunganisha umeme majumbani maofisi viwandani na kadhalika
Kampuni hizo ni kama JBE, IGNITE power nk, wateja wana uhuru wa kuchagua kati ya kampuni hizo ili kupata huduma hiyo ya umeme kwa malipo nafuu au tofauti kulingana na maeneo waliopo
Sielewi kama hali hii niliyozungumzia hapo juu imeshaingia Tanzania na kama imeingia ni njia nzuri na bora kwani inapunguza ukiritimba wa Tannsco kuwa shirika pekee linalozalisha na kusambaza umeme.
Kwa maoni yangu mtuhumiwa ahojiwe vizuri jinsi alivyopata liseni na uendeshaji wa kampuni yake kabla hamjamtuhumu kama mwizi wa umeme
Kwa kufanya hivyo kutawafungua wengi masikio na kama hili halijaingia Tanzania basi kuna haja wawekezaji wazalendo waakishikiana na bunge kuhamasisha kutunga sheria ya kuondoa ukiritimba wa TANNSCO kuzalisha na kusambaza umeme
Wakati huo huo mheshimiwa Otouh CAG ambaye anakagua hesabu za TANNSCO aliangalie na hili ili alitolee tamko
Mungu ibariki Tanzania na watu wake
Hilo na deal la wakubwa wa Tanesco akiwemo huyo Badra,sijui kwa nini yupo mpaka leo. ushauri uliotoa mzuri lakini kamwe nchii haiwezi zingatiwa kwani hii nchi ni Nigeria ya pili watu wanataka maisha bora bila kujituma kufanya kazi,wanatumia bongo zao sana kutaka urahisi na (kwenye siasa URAIS) ili wapate kuiba,sasa ukimwamsha Mtz wao watakula wapi,ndio maana wanaita Bongo land
ReplyDelete