17 August 2012
Vijana watakiwa kutokuwa watumwa wa maandamano
Na Charles Mwakipesile, Mbeya
MWENYEKITI wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mchungaji Nosigwe Buya amewataka vijana nchini kuepuka kuwa sehemu ya kuchafuka kutokana na kutumika mara kwa mara katika maandamano yenye kisingizio cha kudai haki.
Akizungumza na vijana wa kanisa hilo jana, wakati akifunga mkutano wa Wilaya ya Mbeya uliofanyika Songwe Mbeya Vijijini alisema kuwa, kuna kila dalili ya kuona kwa sasa nchini vijana wamekuwa wakitumika kama mtaji wa kudai haki hata kama ikiwa ni kwa kulazimisha kwa kukiuka sheria.
Alisema kuwa, makundi yakiwemo ya kisiasa na wanaharakati wamekwua wakitumia nguvu ya vijana katika mambo ambayo yamekuwa yakiwasababishia hasara kubwa kutokana na baada ya harakati hizo kubaki wakiwa na maisha magumu hivyo kupelekea kuamua kuikatia tamaa nchi yao.
"Vijana ni kundi muhimu linaloweza kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi, kuanzia ngazi ya familia zetu hadi ngazi ya Taifa, lakini hofu yangu ni kuwa vijana wengi wamekuwa wakifundishwa kudai haki kwa nguvu na hivyo kuonesha dalili wazi kuwa wanaweza pia kutumika kwa ajili ya kuwa chanzo cha kumwaga damu," alisema Mchunganji huyo.
Alisema kuwa, vijana hususan waliopo kanisani ni chachu muhimu ya mabadiliko kiuchumi ambayo ikitumika vema ni wazi kuwa hakutakuwa na maandamano na migomo isiyo ya ulazima kutokana na ukweli kuwa kila Mtanzania ataona umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii au kusoma kwa bidii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment