09 August 2012

Ujasiriamali ngao ya kumkomboa mwanamke


Na Jesca Kileo

KATIKA histori ya ya nchi yetu inaonyesha kuwepo kwa uwezo mkubwa wa wanawake kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa na kuleta maendeleo.

Pamoja na kuwepo kwa jitihada hizo bado kumekuwa na vikwazo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa uwezeshwaji kiuchumi kutokana na mila na desturi zilizowafanya wasipelekwe shule ama kubaguliwa katika masuala muhimu ya maendeleo.

Serikali pamoja na juhudi zake za kutoa mikopo kwa wanawake bado kuna asilimia ndogo wanaopata huku makundi yenye uhitaji yakiachwa.

Katika kuhakikisha kuwa maendeleo ya nchi yanapatikana Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha jamii kupiga vita mila na desturi kandamizi ambazo ni kikwazo katika kuwaendeleza wanawake.

Katika suala la elimu, Serikali imefanya jitihada kubwa katika kuhamasisha jamii kuwaandikisha watoto wa jinsia zote shuleni bila ubaguzi na kuweka sheria ndogo za kutekeleza jitihada hizi.

Serikali imefanya jitihada za kujenga shule za msingi kila kijiji na sekondari kila kata ili kuwawezesha watoto wote kupata elimu karibuni na mazingira ya karibu nyumbani.

Katika kuhakikisha kuwa wanawake wanakuwa na maendeleo kwa , Kanisa la Amri Kuu za Mungu (Akuzamu), linaloongozwa na Bw.Edward Amri limekuwa likitoa mafunzo ya mara kwa mara ya ujasiliamali kwa wanawake ili wajikwamua kimaisha.

Katika mafunzo yaliyomalizika hivi karibuni na kuwashirikisha wanawake zaidi 60 kutoka Mkoa wa Dar es Salaam walipata mafunzo namna ya kuendesha biashara zao na kupata faida.

Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na mkufunzu na kuwatunuku vyeti na baada ya kupata mafunzo kwa mwalimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw.Elia Yobu ambapo aliwataka wanawake kutokubali kuachwa nyuma katika suala la kuleta maendeleo nchini.

Akifunga mafunzo hayo Jimbo la Same Mashariki Bi. Anne Kilango Malecela analiwaasa wanawake na kuwataka kuacha kujibweta na kuwategemea wanaume wawatafutir kila kitu.

Anasema kuwa kitendo cha wanawake kuwa ombaomba kwa waume zao huchangia upendo ndani ya nyumba kupungua kutokana na kutojishughulisha.

"Kwa kweli si tabia nzuri kila kitu umtegemee mumeo wakati na wewe una nguvu na akili timamu ni kwanini usijishughulisha na biashara yoyote lafu mkasaidiana ndani ya nyumba kuleta maendeleo?, " alihoji.

Bi. Kilango aliwahimiza kuamka na kuanza kujishughulisha kwa bila ya kuchagua biashara kwani hakuna biashara isiyokuwa na faida isipokuwa kinachohitajika ni usimamizi mzuri.

"Wanawake tumeonekana tunaweza zaidi hivyo ni vyema tukajishughulisha ili kujiingizia kipato na kujiepusha na utafutaji wa pesa kwa njia ambazo zinatudhalilisha jambo ambalo ni kinyume na Mungu, " anasema.

Anasema kuwa ameanza kujifundisha ujasiriamali tangu akiwa na umri mdogo kutokana na mama yake kuwa na biashara ya kuuza kuni na samaki.

Anasema kuwa kutokana na mama yake kuwa na biashara hiyo naye alikuwa akimsaidia ambapo kutokana na mama yake kujishughulisha familia yake ilikuwa na upendo.

Kutokana na elimu hiyo hivyo baada ya kuolewa aliendelea na biashara mbalimbali na kupata faida ambayo hadi sasa anajivunia nayo.

"Ubunge umenikuta nikiwa mjasiriamali na naendelea nayo kwani ndiyo kazi ambayo imenipa manufaa ikiwepo kuwaendeleza kielimu watoto wangu wanne kwa kushirikiana na mume wangu, " anasema.

Pia Bi. Kilango alitumia fursa hiyo kuwaonya wanawake kuacha tabia ya kutoa mitaji yao kwani huchangia kwa asilimia kubwa kurudisha nyuma maendeleo yao.

"Faida ndiyo inayotakiwa kutolewa na ndio maana kuna asilimia kubwa ya wanawake wameshindwa kuendelea na ujasiliamali na kujikuta  wakimwama kwa kutoa mitaji kwa sababu mbalimbali wengine ni baada ya kurubuniwa na waume zao kwa ahadi ya kurejeshwa na matokeo hushindikana, " anasema Bi. Kilango.

Anasema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuwa kuwajengea uwezo ili waweze kuendesha biashara zao kwa faida na kurejesha mikopo wanayopata.

Pia alisema kuwa kutokana na mafunzo hayo wataweza kujiunga pamoja kuanzisha vikundi vya ujasiriamali kama vyama vya SACCOS na Vikoba ambapo itakuwa rahisi kukopa na kurejesha fedha na kuwa na maendeleo.

Anasema kuwa malengo mengine ya mafunzoni hayo ni kuwajengea uwezo ili waweze kuwa na mbinu za kubuni na kuanzisha kuisimamia miradi yao.

"Mjasiriamali ni mtu ambaye ana sifa na uwezo wa
kutambua mapema fursa za kutengeneza faida na mwenye
kuunganisha nguzo kuu za uzalishaji mali (nguvu kazi, mtaji na rasilimali).

Bi. Kilango anasema kuwa majasiriamali ana sifa mbalimbali ikiwemo kuwa mwanzilishi wa wazo na mwenye maono ya mbali ya jinsi ya kufanya biashara, uwezo wa kupanga, kuratibu na kutekeleza wazo lake na kufikia mafanikio pia ni mwenye kujiamini, kujituma kwa muda mrefu, kukubali makosa na kujisahihisha, mbunifu na mwenye kutumia vizuri uwezo na maarifa ya watu wengine.

Anasema kuwa kutokana na juhudi zake alizokuwa akizifanya katika ujasiriamali aliamua kujiingiza kwenye masuala ya siasa na kufanikiwa hadi hapo alipo.

"Safari ya maisha yangu nimetokea mbali kwani nilianza kuuza kunii,chapati, samaki na sasa ni Mbunge wa Jimbo la uchaguzi la Same Mashariki na pia sasa nagombe nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (CWT), " aliongeza kuwa

“Nimeamua kujitokeza kuwania nafasi ya UWT ili niwawakilishe vyema wanawake wenzangu hivyo naomba maombi yenu ili niweze kushinda kiti hiki muhimu”.

Mbunge huyo pia alimpongeza mlezi wa kanisa hilo Bi. Mery Amri kwa kazi ya kuwaelimisha wanawake kuwa wajasiriamali na kuweka utaratibu wa utoaji wa mafunzo kwa ushirikiano na viongozi wenzake.


No comments:

Post a Comment