09 August 2012

Uchaguzi MMFA kufanyika Agosti 18



Na Omary Mngindo, Moshi

CHAMA cha Mpira wa Miguu Manispaa ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro (MMFA), kinatarajia kupata viongozi wake katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Agosti 18, mwaka huu.

Akizungumza mjini hapa jana Msemaji wa Kamati ya Uchaguzi ya MMFA, Barnabas Ndunguru alisema uchaguzi huo utatanguliwa na usaili wa wagombea utakaofanyika Agosti 11, mwaka huu.


Alisema fomu za wagombea zimeshatolewa, ambapo wanamichezo mbalimbali wamejitokeza kuchukua ili kuwania nafasi katika chama hicho.

“Fomu zimeshatolewa kuanzia Julai 20 hadi 27, kipindi cha pingamizi kilikuwa kati ya Julai 28 hadi Agosti 2 na usaili tunatarajia utafanyika Agosti 11 utaofuatiwa na uchaguzi Agosti 18 mwaka huu,” alisema Ndunguru.

Aliwataja wanaowania nafasi katika chama hicho ni Japhet Mpando (Mwenyekiti), Godfrey Madegwa (Makamu Mwenyekiti), Tumaini Madegwa (Katibu Mkuu na Laurance Manyonyi (Katibu Mkuu Msaidizi).

Alisema nafasi ya uwakilishi katika Mkutano Mkuu wa MMFA, inawaniwa na wagombea wanne ambao ni Dalabu Dalabu, Godliva Mushi, Godbless Kimaro na Abdallah Thabit huku nafasi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ikigombewa na Abdallah Mtwende na Idd Manku.

“Nafasi ya Mjumbe wa kuwakilisha klabu kwenda Mkoa inawaniwa na Amry Kiula, Shadrick Lema na Emmanuel Masele ambaye hata hivyo hajarejesha fomu yake,” alisema Ndunguru.

Ndunguru alisema katika kupitia fomu, wamebaini upungufu ambapo waliohusika nao wamepewa taarifa na kurejeshwa kwa walengwa kwa ajili ya marekebisho

No comments:

Post a Comment