09 August 2012
Mwaneti kuhamishia kambi Iringa
Na Amina Athumani
KAMATI ya Michezo ya Walemavu Tanzania (PARALIMPIKI) imeamua kujihami mapema na hali ya hewa ya London, Uingereza inapofanyika michezo ya Olimpiki na PARALIMPIKI ambapo sasa inahamisha kambi mchezaji wake, Zaharani Mwenemti kutoka Zanzibar kwenda Iringa ambako hali ya hewa inafanana kidogo na jiji hilo.
Akizungumza Dar es Salaam juzi, Katibu Mkuu wa PARALIMPIKI Tanzania Idd Kibwana, alisema Mwenemti aliweka kambi Zanzibar kwa mwezi mmoja ili aweze kuzoea hali ya hewa ya kawaida lakini sasa wanaihamishia Iringa.
Alisema mchezaji huyo atafanya mazoezi Iringa hadi Agosti 21, mwaka huu na baada ya hapo atakwenda Dar es Salaam ajili kufanya safari ya London kwa ajili ya michezo hiyo ya Olimpiki kwa upande wa PARALIMPIKI.
Kibwana alisema kijiji cha michezo ya PARALIMPIKI kitafunguliuwa rasmi Agosti 23, mwaka huu mara baada ya kufungwa kwa michezo ya Olimpiki inayoendelea jijini humo.
Alisema Mwenemti, ataondoka nchini Agosti 22, mwaka huu kwenda kwenye michezo hiyo ambayo atashiriki kurusha visahani na tufe.
Katibu huyo alisema michezo ya PARALIMPIKI, itaambatana na Mkutano Mkuu wa viongozi wa kamati hiyo kutoka nchi mbalimbali duniani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment