16 August 2012

Twite kuichezea Yanga Jumapili



Na Mwandishi Wetu

BAADA ya Klabu ya Yanga, kumsajili Mbuyiu Twite wa APR wiki iliyopita beki huyo Jumapili ataichezea timu yake hiyo mpya kwenye Uwanja wa Taifa kwa mara ya kwanza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Celina Chang'a, ambaye ni mmoja kati ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Vannedrick(T) ambao wameshirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kuiandaa mechi hiyo, ileleza kuwa timu hizo zitauchukulia mchezo huo kujiandaa na Ligi Kuu Bara.

Alisema Yanga imepanga kuwatumia baadhi ya nyota wao wapya akiwemo, Twite aliyesajiliwa kutoka APR ya Rwanda na Didier Kavumbayu,
aliyetokea timu ya Atletico ya Burundi.

Tayari kocha wa timu hiyo, Tom Sainfiet ameeleza kuwa amefurahia ujio
wa wachezaji hao ambao amependekeza wasajiliwe ndani ya kikosi chake,
kitu ambacho viongozi wa klabu hiyo wamefanikiwa kukifanya.

Sainfiet alieleza kwamba baada ya kikosi chake kufanya mazoezi kwa
karibu wiki mbili baada ya kufanikiwa kutwaa Kombe la Kagame, tayari
amewapa nafasi wachezaji ambao hawakuwemo kwenye mashindano
hayo.

Kwa upande wa Africa Lyon, wamekiri kuwepo mechi hiyo ambapo Mkurugenzi wake, Karim Kangezi ameeleza kwamba siku hiyo watamtambulisha kocha wao
mpya, Pablo Ignacio Velez kutoka Argentina na wachezaji watatu kutoka
nje ya nchi.

Licha ya jambo hilo, Kangezi alisema kuwa watamtambulisha Mkurugenzi
wao mpya ambaye ni mwanamke na kuweka historia ya kuwa klabu ya kwanza
kuongozwa na mwanamama.

Katibu wa Yanga, Mwesigwa Celestine amethibitisha kuwepo kwa mchezo huo
na kuwataka mashabiki wa timu hiyo kufika kwa wingi kuona wachezaji
hao wapya na kikosi cha timu hiyo kwa ujumla

No comments:

Post a Comment