09 August 2012

TANESCO mapambano dhidi ya vishoka yawe endelevu



JANA baadhi ya vyombo vya habari likiwemo gazeti hili,vilichapisha na kutangaza habari zilizohusu maofisa wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wakishirikiana na Jeshi la Polisi kufanikiwa kukamata kampuni iliyokuwa ikijihusisha na usambazaji wa umeme kinyume cha sheria.

Kampuni hiyo iliyokamatwa katika msako maalumu uliofanyika juzi eneo la Mwananyamala inajulikana kwa jina la Low Voltage Distribution ilikuwa ikijihusha na uuzaji wa umeme huo mali ya TANESCO kwa kutumia njia zisizo halali.

Wakati wa msako,vitendea kazi mbalimbali mali ya shirika la TANESCO kama vile mita za luku, kadi za maombi ya wateja,sare,kamba za kupandia juu ya nguzo,rakiri na vinginevyo vingi vilikutwa ndani ya ofisi hiyo ya usambazaji umeme.

Akizungumza na waandishi habari katika eneo la tukio,Meneja Mahusiano wa shirika la TANESCO,Bi.Badra Masoud,alisema shirika hilo linaendesha msako kama huo nchi nzima kwa lengo la kubaini watu  wote wanaolihujumu.

Alisema hadi sasa watu zaidi ya 50 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo za kuuza umeme wa shirika hilo kwa njia zisizo halali, ambapo aliwataka hata wateja waliouziwa umeme na watu hao nao kujisalimisha mapema kabla ya kukutwa na ‘’fagio la chuma.’’

Tunaunga mkono juhudi zinazofanywa na TANESCO kuwasaka watu wote wanaojihusisha na hujuma dhidi ya shirika hilo zinazolenga kukwamisha mipango yake ya maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Tunaamini msako huo ndiyo njia pekee inayoweza kuwakomboa Watanzania, kwani huenda ukasaidia kukomesha kuwepo kwa vitendo vya namna hiyo nchini na hivyo kuondokana na mgao wa umeme unaozorotesha shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Ni dhahiri kuwa watu hawa huenda wana mtandao mkubwa katika maeneo mengi nchini na si kwa Dar es salaam pekee,hivyo wakiachwa wataliingiza taifa gizani kutokana na shirika hilo kushindwa kujiendesha kutokana na kupata hasara.

Kwa hili tunahitaji kushirikiana na maofisa wa shirika hilo katika mapambano hayo ambayo tunaamini yatakuwa endelevu hadi ushindi utakapopatikana. Kwa msingi huo, hilo si jukumu la TANESCO bali wadau wote wanaoguswa na athari zinazotokana na mgawo wa umeme.

Tunaishauri TANESCO, kwa nia yake nzuri iliyoonesha kuhakikisha inawakomboa Watanzania kiuchumi kwa kuwapatia umeme wa uhakika, baada ya kusambaratisha mtandao wa vishoka.





No comments:

Post a Comment