21 August 2012
Polisi Mwanza kupunguza ajali za barabarani
Na Daud Magesa, Mwanza
JESHI la Polisi mkoani Mwanza, Kikosi cha Usalama Barabarani, kimeandaa mikakati mbalimbali ya kupunguza ajali za barabarani kwa kuacha kufanya kazi kulingana na matakwa ya wanasiasa.
Kamanda wa Kikosi hicho, Mrakibu wa Polisi, Nuru Selemani, alisema ajali nyingi zinazotokea barabarani zinasababishwa na usimamizi mbovu wa sheria, uendesheshaji mbaya wa magari na
uelewa mdogo wa abiria.
Alisema pamoja na jeshi hilo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara, yapo makosa ya kibinadamu ambayo yanakwamisha juhudi hizo kutokana na madereva kushindwa kuzingatia sheria za usalama.
“Ajali nyingi zinazotokea nchini, zinachangiwa na mambo matatu, kwanza usimamizi mbovu wa sheria zetu unaofanywa na watu waliopewa dhamana, uendeshaji mbaya wa vyombo vya usafiri na abiria kutokuwa na uelewa.
“Mbali na makosa ya kibinadamu, ajali nyingi pia zinatokana na sheria zetu za usalama barabarani kupitwa na wakati kwani zimeanza kutumika tangu enzi ya mkoloni hivyo zinahitaji kuboreshwa ili kukidhi matakwa na mahitaji ya sasa,” alisema.
Ili kupunguza ajali mkoani hapa, Kamanda Selemani alisema hivi sasa wameimarisha ukaguzi wa magari ili kuona kama yanakidhi matakwa ya kisheria kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti, Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA).
Aliwaonya abiria kucha kupanda mabari ambayo yamejaza kupita uwezo wake ili kuepusha ajali na kuepuka usumbufu wa kushushwa njiani kwa magari ambayo yatakamatwa na kosa hilo.
“Magari ambayo yatakamatwa kwa kubeba abiria, wamiliki wake watatozwa faini kwa kukiuka sheria, hatuwezi kuangalia uvunjifu wa sheria ukifanyika na kusababisha vifo vya wananchi, lazima tuchukue hatua stahiki,” alisema.
Alisema lipo tatizo la baadhi ya watendaji serikalini na wafanyabiashara wa vyombo vya usafiri kufanya kazi kisiasa badala ya kufuata sheria ili kuepuka adhabu na kuwataka abiria kufunga mikata wawapo safarini.
“Kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu, ajali 240 zimetokea mkoani hapa na kusababisha vifo 110, majeruhi 105 ukilinganisha na mwaka 2011, ambapo ajli zilikuwa 335.
“Mwaka huu zimepungua kwa asilimia 95, katika ajali za mwaka jana, watu 129 walipoteza maisha na majeruhi 132,” alisema na kuongeza kuwa, mwaka 2011, waendesha pikipiki 18 walifariki dunia katika ajali za barabarani.
Alisema hadi kufikia Juni mwaka huu, waendesha pikipiki 24 walifariki dunia katika ajali hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment