24 August 2012

Papaa Msofe aumwa, kesi yaahirishwa



Na Grace Ndossa

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana imeshindwa kusikiliza kesi inayomkabili mfanyabiashara maarufu jijini hapa, Bw. Marijani Msofe (50), maarufu 'Papa Msofe', kwa sababu mshtakiwa anaumwa.

Wakili wa Serikali Bi. Mwanaisha Komba, mbele ya Hakimu Agness Mchome, alidai shuari hilo lilikuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa na upepelezi haujakamilika.

Baada ya Bi. Komba kutoa maelezo hayo, Ofisa mmoja wa Jeshi la Magereza alidai mshtakiwa Bw. Msofe anasumbuliwa na malaria pamoja na kuonesha cheti chake cha hospitali.

Hakimu Mchome aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 4-5 mwaka huu na itasikilizwa mfululizo. Awali wakili wa Serikali Bi. Tumaini Kweka, alidai mshtakiwa ambaye ni mkazi wa Mikocheni, anakabiliwa na kosa moja la mauaji.

Bi. Kweka alidai kuwa, Novemba 6,2011, huko Magomeni Mapipa, mshtakiwa ambaye anatetewa na wakili wa kujitegemea, Bw. Majura Magafu, alimuua Bw. Onesphory Kitoli, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

No comments:

Post a Comment