24 August 2012
Nyilawila ajichimbia Mbeya
Na Mwali Ibrahim
BONDIA Karama Nyilawila, ameamua kuhamishia kambi yake mkoani Mbeya akiwa na lengo la kujiandaa vizuri na pambano lake dhidi Francis Cheka.
Mabondia hao wanatarajia kutwangana Septemba 29, mwaka huu uzito wa kg. 76 ubingwa wa UBO katika Ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Awali Karama aliweka kambi katika gym ya 'Lazima Ukae' iliyopo Sinza Makubirini, Dar es Salaam.
Akizungumza kwa simu akiwa Mbeya, Nyilawila alisema ameamua kuhamisha kambi hiyo kwa kuwa ni nyumbani kwao na pia hali ya hewa nzuri kwa ajili ya kujiandaa.
"Huku ni kwetu na unajua nyumbani ni nyumbani, lakini pia kukaa huku kutanisaidia kujiandaa kikamilifu ili kumtwanga Cheka.
"Naamini Cheka hana ubavu kwangu na ni bondia ambaye huwa ananiogopa mara kwa mara, lakini pia kubadilisha hali ya hewa kunaniongezea uwezo wa kujiandaa vizuri," alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment