24 August 2012
Kingoile apeta usaili Kilimanjaro
Na Elizabeth Mayemba
ALIYEWAHI kuwa kiongozi wa zamani wa Klabu ya Villa Squad, Ally Kingoile amepita katika usaili wa wagombea uongozi katika Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kilimanjaro, ambapo anagombea nafasi ya Katibu Msaidizi.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Septemba 9, mwaka huu mjini Moshi.
Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana akiwa Moshi, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi mkoani humo, Dkt. Haule alisema jumla ya wagombea 13 wamepita katika usaili uliofanyika juzi.
"Usaili ulifanyika kwa amani kabisa na wagombea wote waliopita walitimiza vigezo vinavyotakiwa na Kamati ya Uchaguzi iliridhika," alisema Haule.
Aliwataja wagombea wengine mbali ya Kingoile kuwa Mwenyekiti ni Godluck Moshi na Charles Mchau, Makamu Shaaban Mwalimu, Katibu Mkuu Mussa Mohammed, Mhazini Kusianga Kiata, Mjumbe Mkutano Mkuu Dustin Kilua na Abdallah Hussein.
Mwakilishi wa klabu ni Kenneth Essau na Amri Kiula, Wajumbe Kamati ya Utendaji ni Denis Joseph, Cuthbert Mushi na Nassor Mushi, mwakilishi wa TWFA Salma Omary.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment