07 August 2012
Mwendesha baiskeli agongwa na kufariki
Na Jesca Kileo
MWENDESHA baiskeli Bw.Iddi Hassani (53), mkazi wa Temeke, Dar es Salaam amekufa baada ya kugongwa na gari.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke Bw.David Misime alisema tukio hilo lilitokea Agosti 4, mwaka huu, saa 6 mchana, Barabara ya Mandela eneo la Vetenari wilayani Temeke.
Kamanda Misime alisema marehemu aligongwa na gari namba T 388 BUR, Scania yenye tela namba T 217 BTV ikiendeshwa na dereva Bw.Robert Julius (26), mkazi wa Mwenge akitokea Sokota kuelekea Tazara alimgonga mwendesha baiskeli aliyetambuliwa huyo.
Alisema marehemu Bw.Hassani alikuwa akitokea upande wa kushoto kuelekea upande wa kulia ghafla aligongwa na gari hilo.
Kamanda alisema marehemu alifariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Temeke.
Maiti imehifadhiwa hospitalini hapo na dereva amekamatwa na upelelezi zaidi unaendelea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment